Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook

1 0 2 /

M U N G U M W A N A

Yesu, Masihi na Bwana wa Wote: Alikufa Sehemu ya 2: Maoni Mbadala Kuhusu Maana ya Kifo cha Yesu

Mchungaji Dkt. Don L. Davis

Kifo cha Yesu kimeeleweka kwa njia mbalimbali katika historia ya Ukristo. Kila moja ya nadharia hizi za upatanisho inalenga katika mwelekeo fulani wa wokovu, na zikichukuliwa kwa pamoja zinatuwezesha kupata ufahamu mkubwa zaidi na uelewa wa umuhimu wa kifo cha Yesu kwa ajili yetu. Kifo cha Yesu na maana yake kimeonwa kuwa 1) kielelezo cha kiadili, 2) udhihirisho wa upendo wa Mungu, 3) udhihirisho wa haki ya Mungu, 4) ushindi dhidi ya nguvu za uovu na dhambi, na 5) kukidhi heshima ya Mungu. Ingawa hakuna nadharia moja kati ya hizo inayoelezea kikamilifu kifo cha Yesu, kila moja ina kweli zinazoweza kuboresha uelewa wetu wa maana na ukweli wake kwa upana mkubwa zaidi. Lengo letu la sehemu hii, Maoni Mbadala Kuhusu Maana ya Kifo cha Yesu , ni kukuwezesha kuona kwamba: • Kifo cha Yesu kimeeleweka kwa njia mbalimbali katika historia yote ya Kikristo. • Kila moja ya nadharia mbalimbali za upatanisho ambazo zimeshamiri katika Kanisa kwa karne nyingi inalenga katika mwelekeo fulani wa wokovu, na zikichukuliwa kwa pamoja zinatuwezesha kupata ufahamu mpana zaidi na uelewa wa kina wa umuhimu wa kifo cha Yesu kwa ajili yetu. • Baadhi ya nadharia kuu kuhusu maana ya kifo cha Yesu ni pamoja na kuona kifo chake kama 1) kielelezo cha kiadili, 2) udhihirisho wa upendo wa Mungu, 3) udhihirisho wa haki ya Mungu, 4) ushindi dhidi ya nguvu za uovu na dhambi, na 5) kukidhi heshima ya Mungu. • Ingawa hakuna nadharia moja kati ya hizo inayoelezea kikamilifu kifo cha Yesu, kila moja ina kweli zinazoweza kuboresha uelewa wetu wa maana na ukweli wake kwa upana mkubwa zaidi.

Muhtasari wa Sehemu ya 2

3

Made with FlippingBook - Online magazine maker