Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook
1 0 4 /
M U N G U M W A N A
2. Tunapaswa kufuata kielelezo cha kifo cha Yesu kwa kuwajali wengine na kuhubiri Habari Njema.
3. Hatupaswi kamwe kurahisisha huzuni ya Yesu kupita kiasi: hakufa kisitiari ili kufundisha somo kwa njia ya mifano, bali alikufa kiuhalisia ili kutukomboa kwa ajili ya Mungu (1 Pet. 3:18).
II. Mtazamo wa pili: Kifo cha Yesu kama udhihirisho wa upendo wa Mungu ( nadharia ya ushawishi wa kimaadili )
Ndugu zangu, msiseme neno
lolote baya dhidi ya yule aliyesulubiwa. Usidharau mapigo ambayo kwayo kila mtu anaweza kuponywa, kama vile sisi [Wakristo] tunavyoponywa. ~ Justin Martyr (c. 160, E), 1.268. Ibid. uk. 42.
A. Waandishi na hoja za wale wanaoshikilia mtazamo wa Ushawishi wa Kimaadili :
1. Watetezi wa mtazamo huu:
3
a. Peter Abelard
b. Horace Bushnell (1802-1876)
2. Mungu ni pendo: haki, ghadhabu, kisasi na utakatifu wake si tatizo letu kuu, bali mtazamo wetu kwake .
3. Ugumu wa kuwa katika ushirika na Mungu upo ndani yetu, si katika Mungu mwenyewe .
a. Hatuujui upendo wake kwetu.
b. Hatuelewi kwamba dhambi yetu imemletea huzuni.
Made with FlippingBook - Online magazine maker