Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook
/ 1 1 3
M U N G U M W A N A
3. Kifo cha Yesu pekee ndicho kinaweza kututatulia mtanziko wa dhambi; hakuna kiasi cha marekebisho ya kimaadili au huzuni ya kimungu kinachotatosha (Gal. 3:11-13).
VI. Mawazo ya kuhitimisha kuhusu ya maoni tofauti ya upatanisho
A. Maoni yote yana vipengele vya ukweli.
1. Kifo cha Yesu kilitutolea kielelezo cha maana ya kuishi kwa ajili ya Mungu.
2. Kifo cha Yesu kilionyesha upendo wa Mungu kwetu.
3
3. Kifo cha Yesu kilifunua matokeo ya kutisha ya dhambi, na kuonyesha matakwa matakatifu ya Mungu katika sheria na utawala wake.
4. Kifo cha Yesu kiliharibu nguvu za Shetani na kifo, na kuwaweka huru watu wa Mungu ili waishi huru katika Kristo.
5. Kifo cha Yesu kilitosheleza utakatifu na heshima ya Mungu kuhusiana na dhambi na makosa yetu.
B. Hakuna mtazamo mmoja unaofafanua kwa ukamilifu upana na kina cha ufunuo wa kile ambacho Yesu alitimiza pale Kalvari.
C. Ni Maandiko pekee yanayoweza kutoa ufahamu wa wazi, wa mwisho na wa kiukombozi kuhusiana na maana ya kifo cha Yesu.
Made with FlippingBook - Online magazine maker