Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook
1 1 2 /
M U N G U M W A N A
B. Hoja dhidi ya mtazamo wa Kuridhika :
1. Una mawazo ya kuvutia: unakubaliana vizuri sana na jukumu la Kristo kama mpatanishi kamili kati ya Mungu na wanadamu, anayeweza kukidhi matakwa ya Mungu kwa dhambi zetu.
a. Alilipa deni letu kwa hiari (Yohana 10:17-18).
b. Alitosheleza heshima ya Mungu kwa niaba yetu (kama mbadala), Ebr. 2:9.
2. Lugha hii ni yenye maana kubwa: lugha ya kuridhika kwa hakika ni kipengele muhimu katika maana ya kifo cha Kristo (1 Yohana 2:2).
3
3. Huelekea kupunguza maana ya kifo cha Yesu kana kwamba ni matakwa ya kisheria, vipengele vingine vingi vya kifo cha Kristo havionekani kuangaziwa vya kutosha au kupewa umaana mwingi katika mtazamo huu.
C. Tunaweza kupata kweli gani kutokana na mtazamo huu?
1. Kifo cha Yesu kinatosheleza kwa ukamilifu wote madai ya haki ya Mungu dhidi yetu kwa sababu ya kosa la dhambi zetu kwa Mungu (Rum. 5:9-11).
2. Thamani ya kifo cha Yesu haina kikomo; kifo chake kina nguvu sana kiasi kwamba alikufa mara moja tu na kutosheleza dhabihu iliyohitajika kwa ajili yetu (Ebr. 10:10-14).
Made with FlippingBook - Online magazine maker