Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook

/ 1 4 3

M U N G U M W A N A

• Kanuni ya Imani inazungumza kwamba Yesu Kristo atarudi tena katika utukufu, tendo ambalo litakuwa la ajabu kwa maana ya ukuu wa tendo lenyewe na lina umuhimu kwa wakati wa sasa katika maisha na huduma zetu. • Kanuni ya Imani pia inathibitisha kwamba atakuja kuhukumu mataifa, kwa maana Baba amemkabidhi Mwana hukumu yote. • Hatimaye, Kanuni ya Imani inakiri kwamba atatawala na Ufalme wake hautakuwa na mwisho, atatimiza unabii wa Agano la Kale na kuanzisha utawala wa Mungu katika mbingu mpya na nchi mpya. • Kweli hizi tatu (yaani, kuja kwake katika utukufu, hukumu yake kwa mataifa, na Ufalme wake wa milele) zinabeba maana kubwa katika maisha na huduma zetu leo. Kama katika kipindi chetu kilichopita, hebu tusome kipengele husika cha Kanuni ya Imani kinachohusiana na somo letu la mwisho: “Siku ya tatu alifufuka kama yasemavyo Maandiko, akapaa mbinguni na ameketi mkono wa kuume wa Baba. Atarudi tena katika utukufu, kuhukumu walio hai na wafu, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho.”

Muhtasari wa sehemu ya 2 ya video

4

I. “Atarudi Tena Katika Utukufu”: Ujio wa Pili wa Yesu Kristo

Anazungumza kuhusu siku ya kutokea kwake,

wakati atakapokuja na kutukomboa, kila mmoja kwa kadiri ya matendo yake. ~ Klementi wa Pili (c. 150), 7.522. David W. Bercot, ed. A Dictionary of Early Christian Beliefs . Peabody, MA: Hendrickson Publishers, 1998. uk. 606.

A. Kuja kwake kutakuwa halisi (Yesu Masihi mwenyewe atarudi).

1. Atakuja ili kutupeleka kwake (Yohana 14:3).

2. Bwana mwenyewe atashuka (1 Thes. 4:16-17).

3. Hakunawawakilishi,mbadala, auwajumbewatakaokuja ili kukamilisha Ufalme wa Mungu. Yesu atakuja mwenyewe, binafsi, nasi tutauona utukufu wake (Yohana 17:24).

Made with FlippingBook - Online magazine maker