Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook

/ 1 5

M U N G U M W A N A

Yesu, Masihi na Bwana wa Wote Alikuja

S O M O L A 1

Karibu katika Jina lenye nguvu la Yesu Kristo! Baada ya kusoma, kujifunza, kushiriki katika mijadala, na kutendea kazi yaliyomo katika somo hili, utakuwa na uwezo wa: • Kueleza umuhimu wa Kanuni Imani ya Nikea katika elimu ya Kristo (Kristolojia). • Kufafanua kwa umakini mada ya Kristolojia na kuongelea umuhimu wake kwa ujumla katika kuandaliwa kwetu kama viongozi katika Kanisa. • Kuonyesha kwa usahihi jinsi Kanuni ya Imani ya Nikea inavyosaidia kuboresha fikra zetu kama wahudumu wa mijini, kuhusiana na kujifunza kwetu maarifa ya kibiblia juu ya Yesu. Hili ni muhimu hasa katika maana ya kutusaidia kuiona kazi ya Kristo katika sura mbili: kunyenyekezwa kwake (yaani, kufanyika kwake mwanadamu na kufa kwake msalabani kwa ajili yetu), na kuinuliwa kwake (kufufuka kwake, kupaa kwake, na tumaini la kurudi kwake katika nguvu). • Kuelezea njia ambazo somo la Kristolojia linaweza kuwa msaada wa pekee sana leo kwa watu kama sisi tunaofanya kazi katika jamii za mijini, kuona namna ambavyo ufahamu mpya juu ya Kristo unavyoweza kutuwezesha kuudhihirisha vyema zaidi na upendo wa Mungu kwa wanadamu, na ahadi yake tukufu ya ufalme. • Kuelezea kwa usahihi vipengele muhimu vya asili ya Yesu kabla hajaja duniani, kama Neno au Logos aliyekuwepo hapo awali, kwa kutumia Kanuni ya Imani ya Nikea kama ufunguo wa kuuelewa uungu wa Yesu. • Kuonyesha njia tatu tofauti ambazo uwepo wa Yesu unaonekana katika Maandiko: kwanza kama Mungu Mwana, nafsi ya kiungu aliye sawa na Mungu, kama Yule Anayetarajiwa katika unabii wa Agano la Kale kuhusu Masihi, na kisha kama Neno la Mungu Aliyefanyika Mwili, Mungu katika umbo la mwanadamu. • Kutoa maelezo ya kukanusha uzushi mkuu wa kihistoria kuhusu uungu wa Kristo, na kutoa maoni juu ya umuhimu wa uungu wa Yesu kwa imani yetu na ufuasi.

Malengo ya Somo

1

Made with FlippingBook - Online magazine maker