Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook

1 6 /

M U N G U M W A N A

Bwana wangu na Mungu wangu!

Ibada

Yohana 20:19-29 - Ikawa jioni, siku ile ya kwanza ya juma, pale walipokuwapo wanafunzi, milango imefungwa kwa hofu ya Wayahudi; akaja Yesu, akasimama katikati, akawaambia, Amani iwe kwenu. 20 Naye akiisha kusema hayo, akawaonyesha mikono yake na ubavu wake. Basi wale wanafunzi wakafurahi walipomwona Bwana. 21 Basi Yesu akawaambia tena, Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi. 22 Naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu. 23 Wo wote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; na wo wote mtakaowafungia dhambi, wamefungiwa. 24 Walakini mmoja wa wale Thenashara, Tomaso, aitwaye Pacha, hakuwako pamoja nao alipokuja Yesu. 25 Basi wanafunzi wengine wakamwambia, Tumemwona Bwana. Akawaambia, Mimi nisipoziona mikononi mwake kovu za misumari, na kutia kidole changu katika mahali pa misumari, na kutia mkono wangu katika ubavu wake, mimi sisadiki hata kidogo. 26 Basi, baada ya siku nane, wanafunzi wake walikuwamo ndani tena, na Tomaso pamoja nao. Akaja Yesu, na milango imefungwa, akasimama katikati, akasema, Amani iwe kwenu. 27 Kisha akamwambia Tomaso, Lete hapa kidole chako; uitazame mikono yangu; ulete na mkono wako uutie ubavuni mwangu, wala usiwe asiyeamini, bali aaminiye. 28 Tomaso akajibu, akamwambia, Bwana wangu na Mungu wangu! 29 Yesu akamwambia, Wewe, kwa kuwa umeniona, umesadiki; wa heri wale wasioona, wakasadiki. Kabla ya sisi kama viongozi na watumishi wa Kristo kumtumikia Bwana wetu kwa kuwatumikia wengine, kwanza kabisa na zaidi ya mambo yote, sisi ni watu wa ibada. Kumpenda Bwana Mungu wetu ndio Amri Kuu na ya kwanza (taz. Mt. 22:30 na kuendelea), na wale wanaompenda Bwana kweli bila masharti wataleta athari njema katika familia zao na kwa marafiki, washirika na wafanyakazi wenza, majirani, na hata maadui zao. Kiini cha aina hii ya athari ni nini? Katika kisa hiki, Tomaso aitwaye Pacha, mmoja wa wanafunzi wa Yesu, anafunua nguvu ya ufunuo wa kweli wa Yesu Kristo katika kuleta matokeo. Akiwa amejaa hofu na mashaka kwa sababu hakuwepo wakati Kristo alipowatokea wanafunzi wake baada ya kufufuka, Tomaso asema kwa msisitizo kwamba hataamini pasipo uthibitisho thabiti wa kisayansi wa ufufuo wa Bwana. Akiwa na uzito na kusita kwingi kukumbatia ushuhuda wa wanafunzi wenzake, aliweka wazi kigezo cha uthibitisho ambao ungeishurutisha imani yake. “ Nisipoziona mikononi mwake kovu za misumari, na kutia kidole changu katika mahali pa misumari, na kutia mkono wangu katika ubavu wake, mimi sisadiki hata kidogo .” Kigezo cha juu, kwa kweli, kwa mfuasi mchanga na mgumu! Yesu anatowakea tena wanafunzi, wakati huu Tomaso akiwepo. Yesu anatimiza waziwazi kigezo kilichowekwa na Tomaso: “ Lete hapa kidole chako; uitazame mikono yangu; ulete na mkono wako uutie ubavuni mwangu, wala usiwe asiyeamini, bali aaminiye .” Jibu la Tomaso linaonyesha namna ambavyo mashaka yake juu ya uhalisi wa ufufuo wa Yesu yaliyeyuka katika dakika moja iliyoghubikwa na kutambua, upendo, na

1

Made with FlippingBook - Online magazine maker