Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook
/ 1 5 1
M U N G U M W A N A
B. Hukumu ni ya ajabu .
C. Masuala ya ufalme ni nyeti sana .
D. Utume wetu uko wazi : enendeni mkafanye wanafunzi wa Yesu katika mataifa yote haraka iwezekanavyo, Mt. 28 :18-20.
Wakati wa kuja kwake, ni wenye haki tu ndio watafurahi. Kwa maana wanatazamia mambo ambayo wameahidiwa. Na muendelezo wa mambo ya dunia hautadumishwa tena. Badala yake, vitu vyote vitaharibiwa. ~ Mzozo wa Archelaus na Manes (c. 320, E), 6.2111. Ibid. uk. 606.
Hitimisho
» Vifungu vitatu vya mwisho katika sehemu ya Kristolojia ya Kanuni ya Imani ya Nikea vinazungumza juu ya kuja kwa Kristo katika utukufu, hukumu yake inayokuja kwa watu wote, na utawala wake ujao wa milele. » Kwa sababu Bwana wetu Yesu amefufuka na kuinuliwa, anastahili ibada yetu ya juu na utumishi bora zaidi. » Lazima tujitahidi kumfanya ajulikane, katika kunyenyekezwa na kuinuliwa kwake, katika vitongoji vyetu, miji yetu, na ulimwengu mzima kwa kuwa Yeye peke yake ndiye Bwana, na Yeye pekee ndiye atakayetawala. Maswali yafuatayo yaliundwa ili kukusaidia kupitia maarifa yaliyomo katika sehemu ya pili ya video. Kanuni ya Imani ya Nikea inatupatia muhtasari ulio wazi na wenye nguvu wa ushuhuda wa Biblia kuhusu kuja kwa Kristo katika utukufu, hukumu yake inayokuja kwa watu wote, na utawala wake ujao wa milele. Ni muhimu sana kwako kuwa na ufahamu wa elimu hii, katika suala la ufuasi wako binafsi, na ni muhimu vile vile kwa ushuhuda wako na huduma. Pitia yaliyomo katika sehemu hii kupitia maswali haya, na uthibitishe jibu lako kwa ushahidi thabiti wa Biblia. 1. Ni zipi sifa za Ujio wa Pili wa Yesu Kristo? Kwa nini ni lazima kutangaza kwamba kuja kwake kutakuwa halisi na kwa kuonekana (rej. Mdo. 1:11)? Je, viumbe wa kimalaika watakuwa na jukumu gani katika ujio wake mtukufu? 2. Nini maana ya ukweli kwamba kuja kwa Bwana kutakuwa kwa ghafla na pasipo kutazamiwa ? Je, hii inamaanisha nini kuhusu mienendo ya sasa ya makongamano ya unabii na semina za kutabiri ujio wa Kristo? Utukufu wote ni kwa Jina lake. Amina!
4
Sehemu ya 2
Maswali kwa wanafunzi na majibu
Made with FlippingBook - Online magazine maker