Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook
1 5 0 /
M U N G U M W A N A
c. 1 Wakorintho 3:22-23
d. Ufunuo 2:26-27
e. Ufunuo 3:21
C. Mara tu maadui wote wanapokuwa wametiishwa chini ya miguu ya Kristo, kutia ndani kifo, basi Kristo atakabidhi Ufalme kwa Mungu, ambaye atakuwa Yote katika yote katika ulimwengu wote. 1 Wakorintho 15:24-25, 28 – Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu. 25 Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke maadui wake wote chini ya miguu yake. 28 Basi, vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake, ndipo Mwana mwenyewe naye atatiishwa chini yake yeye aliyemtiishia vitu vyote, ili kwamba Mungu awe yote katika wote.
1. Kristo atakabidhi utawala wa ufalme kwa Mungu.
4
2. Mungu atakuwa Yote katika yote.
IV. Kweli Zinazohusu Kurudi kwa Yesu Kristo
Isaya 62:11 – Tazama, Bwana ametangaza habari mpaka mwisho wa dunia, Mwambieni binti Sayuni, Tazama, wokovu wako unakuja; Tazama, thawabu yake i pamoja naye, Na malipo yake yako mbele zake. Ufunuo 22:12-13 - Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. 13 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.
A. Kuja kwake ni hakika .
Made with FlippingBook - Online magazine maker