Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook
/ 1 9
M U N G U M W A N A
kuhusiana na mambo madogo madogo ya kimafundisho. Badala ya kujikita katika mijadala isiyo na afya na ya kuchosha kuhusu migogoro ya kitheolojia ya siku za kale, tunahitaji kujihusisha na kujiwekeza katika masuala muhimu ya muktadha na wakati wetu. Hoja yao ni rahisi na ya kueleweka. Kwa kuwa watu wengi hawajali sana kuhusu migogoro ya kale ambayo walikuwa nayo watu fulani kuhusiana na asili na maisha ya Kristo, ambao historia zao hazifahamiki vizuri sana leo, pengine hatupaswi kutumia muda mwingi kwenye mimbari na mawasilisho yetu juu ya hayo. Tunahitaji kuzungumza mambo ya uhakika, ya kisasa, na yenye umuhimu katika zama hizi. Wengine, wakiwa na msimamo tofauti, wanaamini kwamba kujifunza mafundisho ya Kikristo ndio msingi wa ibada, ushirika, na huduma zetu zote. Pasipo kuifahamu kweli kuhusu Kristo alikuwa nani hasa, ni nani, na atakuwa nani, hatuwezi kueneza Injili ifaavyo wala kuhudumia ulimwengu usio na Mungu. Kwa maoni yako, ni hoja ipi yenye mantiki zaidi kati ya hoja hizi?
1
Yesu, Masihi na Bwana wa Wote: Alikuja Sehemu ya 1: Dibaji ya Elimu Juu ya Kristo
YALIYOMO
Mchungaji Dkt. Don L. Davis
Kanuni ya Imani ya Nikea inatoa muhtasari kwa uwazi na kwa ufupi unaotupa ufahamu juu ya Yesu Kristo na kazi yake. Fundisho la Kristo, au “Kristolojia,” linahusisha uchunguzi wa kina wa Maandiko ya Biblia kuhusu Yesu, hasa katika maana ya kutusaidia kuiona kazi ya Kristo katika sura mbili: kunyenyekezwa kwake (yaani, kufanyika kwake mwanadamu na kufa kwake msalabani kwa ajili yetu), na kuinuliwa kwake (kufufuka kwake, kupaa kwake, na tumaini la kurudi kwake katika nguvu). Yesu Kristo ndiye msingi wa imani ya Kikristo (1Kor. 3:11). Ukristo umejengwa juu ya upekee, kwa hakika uungu, wa Yesu wa Nazareti. Kukubali fundisho hili la msingi la Maandiko kunaufanya mfumo mzima wa Kikristo wa umwilisho, miujiza, upatanisho, na ufufuo ulete maana nzuri sana. Kuikataa kweli hii kuu kunaifanya imani iporomoke na kuingia katika mkanganyiko. Wakristo wanaweza kutofautiana juu ya namna ya ubatizo, juu ya nafasi ya wanawake katika kanisa, au juu ya maelezo ya unabii. Lakini Wakristo wa kweli, bila kujali madhehebu yao, wanakubaliana kwamba kila kitu kinategemea uungu wa Kristo.
Muhtasari wa Sehemu ya 1
~ Bruce Demarest, Jesus Christ: The God-Man . Eugene, OR: Wipf and Stock Publishers, 1978. p. 28.
Made with FlippingBook - Online magazine maker