Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook
2 0 /
M U N G U M W A N A
Lengo letu katika sehemu hii, Dibaji ya Elimu Juu ya Kristo , ni kukuwezesha kuona kwamba: • Kanuni ya Imani ya Nikea ina umuhimu mkubwa kwetu tunapochunguza kile ambacho Maandiko yanafundisha kuhusu Kristo, kwa lugha rasmi “Kristolojia.” • Fundisho la Kristolojia lina umuhimu mkubwa katika mafunzo yetu kama viongozi katika Kanisa, hasa kwa jinsi linavyosaidia kuweka msingi thabiti wa uelewa wetu wote wa hadithi na imani ya Kikristo. • Kanuni ya Imani ya Nikea inatengeneza fikra zetu kuhusiana na Yesu na kazi yake, hasa katika namna inavyounda mtazamo wetu kwa habari ya kazi ya Kristo kama mitazamo miwili inayohusiana : kunyenyekezwa kwake (yaani, kufanyika kwake mwanadamu na kufa msalabani kwa ajili yetu) na kuinuliwa kwake (kufufuka kwake, kupaa kwake, na tumaini la kurudi kwake katika nguvu). • Elimu mpya ya Kristolojia inaweza kuwawezesha watenda kazi na wahudumu Wakristo wa mijini kudhihirisha vyema zaidi upendo wa Mungu kwa wanadamu, na kutoa ushahidi wa kuvutia zaidi kuhusu ahadi yake tukufu ya ufalme.
1
I. Umuhimu wa Kanuni ya Imani ya Nikea katika Elimu ya Kristolojia
Muhtasari wa Sehemu ya 1 ya Video
A. Ufafanuzi wa Kristolojia
1. Christos = Masihi, Kristo, mpakwa mafuta; logos = elimu ya, maarifa ya
2. Nafsi ya Kristo ni kitovu cha imani ya Kikristo kwa namna ya kipekee tofauti na dini nyingine. Uhusiano wa karibu wa Kristo na Ukristo ni mojawapo ya sifa bainifu za dini ya Kikristo. Ukiondoa jina la Buddha kutoka kwenye Ubuddha na kumuondoa mjumbe wake katika mfumo wa imani hiyo; kama utamuondoa Muhammad kutoka kwenye Uislamu, au Zoraster kutoka kwenye dini ya kihajemi ya zamani, fundisho zima la dini hizi bado litabaki salama. Thamani ya kimatendo ya dini hizi, kama ilivyo, isingehatarishwa au kupunguzwa. Lakini muondoe Yesu Kristo kwenye Ukristo, utaacha nini? Hakuna kitakachobaki!
Made with FlippingBook - Online magazine maker