Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook

/ 2 3 3

M U N G U M W A N A

Kiini na Chimbuko: Ukristo Ni Yesu Kristo (muendelezo)

• Ambaye alikufa kwa aibu, aliuawa hadharani kati ya wezi wawili, na kuwekwa kwenye kaburi la kuazimwa. Hata hivyo watu wote, vitabu, falsafa, mifumo, serikali, wasanii, waelimishaji, viongozi wa kidini, washindi wa kijeshi, watu wenye ushawishi na mamlaka wakiwekwa pamoja hawajapata matokeo kama ambayo mhubiri huyu mmoja wa Kiyahudi amekuwa nayo juu ya muundo na hatima ya Dunia. Ukristo ni Yesu Kristo. Hadithi hii inahusu maisha yake na ushawishi na wito na maono na kazi na siku zijazo. Ili kuelewa yote ambayo Mungu anataka tujue na tuwe na tufanye, tunachopaswa kufanya ni kuwa na ujuzi wa kina kuhusu maisha na utu wa Kristo, ambaye wafuasi wake wanakiri kuwa yu hai leo. Wakolosai 1:15-20 - naye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote. 16 Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake. 17 Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye. 18 Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote. 19 Kwa kuwa katika yeye ilipendeza utimilifu wote ukae; 20 na kwa yeye kuvipatanisha vitu vyote na nafsi yake akiisha kufanya amani kwa damu ya msalaba wake; kwa yeye, ikiwa ni vitu vilivyo juu ya nchi, au vilivyo mbinguni. Andiko La Leo

I. Yesu, Ufunuo wa Mwisho na Kamili wa Mungu. Ili Kumwelewa Baba, Ni Lazima Tupate Kumjua Yesu Kristo, Ambaye Ndiye Njia na Hatima ya Uumbaji Wenyewe.

A. Yesu ni mfano dhahiri wa nafsi ya Mungu, ambaye kwa Yeye Mungu aliumba ulimwengu wote ulioumbwa. Kol. 1:15-16 - naye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote. 16 Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake.

Made with FlippingBook - Online magazine maker