Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook

2 3 4 /

M U N G U M W A N A

Kiini na Chimbuko: Ukristo Ni Yesu Kristo (muendelezo)

B. Yesu ndiye kiwakilishi kamili cha Mungu (chapa halisi ya asili yake) katika umbo la mwanadamu, Ebr. 1:1-4 - Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, 2 mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu. 3 Yeye kwa kuwa ni mng’ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu; 4 amefanyika bora kupita malaika, kwa kadiri jina alilolirithi lilivyo tukufu kuliko lao. C. Yesu ni Neno aliyefanyika mwili, mfunuaji wa fahari na uzuri wa Mungu. Yohana 1:14 - Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli. Yohana 1:18 - Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua.

D. Nafsi ya Yesu ni picha kamili na isiyoghoshiwa ya tabia na uzuri wa Baba Mungu ambaye tunampenda na kumwabudu. Tunamjua Mungu kupitia yeye.

Wengi wanatosheka kuwa na ujuzi duni na wa kawaida kuhusu Yesu, ambao hauwasaidii kugundua wala kufurahi katika siri iliyomo katika maana ya “Kristo ndani yenu, tumaini la Utukufu.” Wakati wa mahubiri ya watoto Mchungaji Msaidizi aliwauliza watoto, “Kijivu ni nini, ana mkia wenye kichaka na anakusanya karanga katika msimu wa joto?” Mtoto mmoja wa miaka mitano aliinua mkono wake: “Najua jibu linapaswa kuwa Yesu,” alianza, “lakini kwangu kwangu inaonekana kama kindi” ( Reader’s Digest ). • Kwa Wakristo, hakuna maarifa ya wokovu wa Mungu ambayo hayamtambui Yesu Kristo kama mpatanishi pekee, Yohana 14:6.

Made with FlippingBook - Online magazine maker