Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook

2 4 0 /

M U N G U M W A N A

Kiini na Chimbuko: Ukristo Ni Yesu Kristo (muendelezo)

• Petro anasema katika waraka wake wa pili, 2 Petro 3:18 kwamba tunapaswa kukua “katika neema, na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na hata milele.” • Jina lake pekee ndilo tulilopewa chini ya mbingu ili tupate kuokolewa, Matendo 4:12 - Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo. • Yohana Mtume anasema katika waraka wake wa kwanza, 1 Yohana 3:1-3 - Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye. 2 Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo. 3 Na kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa, kama yeye alivyo mtakatifu. D. Kulingana na mapenzi ya Mungu, tumebatizwa (kuwekwa ndani ya na kuzungukwa na) Kristomwenyewe, ambaye ni tumaini letu la utukufu, sasa tuitwa kwamba tu “ndani ya Kristo.” Sisi tunaoamini tumetambulishwa pamoja na Kristo Yesu, na kufanywa sehemu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, ambalo ni “Siri” iliyofichuliwa: siri iliyo wazi ya Mungu. • Warumi 16:25-27, “ufunuo wa siri” • Waefeso 3:7-10, hekima ya Mungu inayodhihirishwa kupitia Kanisa • Wakolosai 1:25-27, Kristo ndani yetu, tumaini la utukufu. E. Yesu ni mtawala wa Mungu, kielelezo cha Mungu, kanuni ya Mungu ya urafiki na kitambulisho kwa waliokombolewa. Kusudi la Mungu ni kumfanya kila mmoja wetu ambaye anaamini afanane na maisha halisi na ukamilifu wa Kristo mwenyewe. Sikiliza kile ambacho Agano Jipya linafundisha kuhusu uhusiano wetu na Bwana wetu. • Tumefanywa “wamoja katika Kristo,” 1 Kor. 6:15-17. • Tulibatizwa katika yeye, 1 Kor. 12:13.

Made with FlippingBook - Online magazine maker