Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook

/ 2 4 1

M U N G U M W A N A

Kiini na Chimbuko: Ukristo Ni Yesu Kristo (muendelezo)

• Tulikufa pamoja naye, Rum. 6:3-4. • Tulizikwa pamoja naye, Rum. 6:3-4. • Tulifufuliwa pamoja naye, Efe. 2:4-7. • Tumepaa pamoja naye, Efe. 2:6.

• Tumeketishwa pamoja naye katika ulimwengu wa roho, Efe. 2:6. • Katika ulimwengu huu, tunajitwika nira yake na kubeba mzigo na msalaba ambao ametukabidhi, Mt. 11:28-30. • Katika ulimwengu huu, tumeitwa kuteseka pamoja naye, Rum. 8:17 18; Fil. 1:29-30. • Iwe tunaishi au tunakufa, sisi ni wa Bwana Yesu kikamilifu, Rum. 14:7-9 - Kwa sababu hakuna mtu miongoni mwetu aishiye kwa nafsi yake, wala hakuna afaye kwa nafsi yake. 8 Kwa maana kama tukiishi, twaishi kwa Bwana, au kama tukifa, twafa kwa Bwana. Basi kama tukiishi au kama tukifa, tu mali ya Bwana. 9 Maana Kristo alikufa akawa hai tena kwa sababu hii, awamiliki waliokufa na walio hai pia.

• Tutatukuzwa pamoja naye, Rum. 8:17. • Tutafufuliwa katika yeye, 1 Kor. 15:48-49. • Tutafanana na yeye, 1 Yohana 3:2. • Sisi ni warithi pamoja naye, Rum. 8:17. • Tutatawala pamoja naye milele, Ufu. 3.

Made with FlippingBook - Online magazine maker