Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook
/ 3 3
M U N G U M W A N A
h. Mwamuzi wa watu wote, Yohana 5:22; 2 Tim. 4:1; Matendo 17:31; Mt. 25:31-46
B. Anayetarajiwa: Unabii wa Kimasihi wa AK
1. Yesu ni uzao wa mwanamke ambaye alitabiriwa kuwa ataponda kichwa cha nyoka, Mwa. 3:15.
1
2. Yesu ni uzao wa Ibrahimu, ambaye kupitia yeye jamaa zote za dunia zingebarikiwa, Mwa. 12:1-3 ( ona pia Mwa. 15:5-6; 17:4-8).
3. Yesu ndiye Kuhani Mkuu mfano wa ukuhani wa milele wa Melkizedeki, Mwa. 14:18-20 na Ebr. 6:20-7.22.
4. Yesu ndiye Mfalme wa Kifalme katika ukoo wa Daudi aliyeteuliwa kutawala milele kama Bwana, Isa. 9:6-7.
5. Yesu kama Mtumishi wa Yehova, Mpakwa mafuta wa Mungu, Isa. 61:1 - na Luka 4:18-19.
C. Aliyechukua Mwili: Neno Aliyefanyika Mwili
1. Neno alifanyika mwili akakaa kwetu (Yohana 1:14-18).
2. Yeye ambaye alikuwa yuna namna ya Mungu ( morphe ) alichukua umbo la mwanadamu, Flp. 2:5-11.
3. Mwana ni mfano wa Mungu asiyeonekana ambaye kupitia yeye vitu vyote viliumbwa, vinashikamana, na vinapata kusudi la kuwepo (Kol. 1:15-20).
Made with FlippingBook - Online magazine maker