Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook
/ 3 7
M U N G U M W A N A
6. Elezea njia ambazo Yesu wa Nazareti anatimiza unabii wa AK kuhusu kuja kwa Masihi. Kwa nini ushahidi huu muhimu unaunga mkono zaidi uwepo wa Yesu tangu awali kama Logos ? 7. Je, ushuhuda wa Yohana kuhusu Umwilisho wa Yesu unatusaidiaje kuelewa uhusiano wake na “ Neno Aliyefanyika Mwili ?” Je, ni kwa jinsi gani tunapaswa kuelewa na kuelezea vyema zaidi fumbo la kuja kwa Mungu kwa namna ya mwanadamu katika nafsi ya Yesu Kristo? 8. Orodhesha kwa umakini mafundisho ya uongo ya makundi mawili ya uzushi wa kihistoria yaliyotajwa katika sehemu yetu ya mwisho, Uzushi wa Kiebioni (Ebionism) na Uzushi wa Ario (Arianism) . Je, ni kwa jinsi gani Kristolojia ya Kiutendaji [Functional Christology] imetafuta kuelezea uhusiano wa Mungu na mwanadamu ndani ya Yesu? 9. Toa sababu kadhaa kwa nini ni muhimu sana kwetu kuelewa na kuthibitisha uungu wa Kristo katika makanisa yetu ya mijini. Kwa nini fundisho hili ni muhimu kwa ufuasi (uanafunzi) wako kibinafsi? Kipande cha nyimbo/maungamo kilichohifadhiwa katikaWaebrania 1:1-4kinamwelezea Yesu kama “mng’ao wa utukufu wake” ( apaugasma tes doxes ) na “chapa ya nafsi yake” ( charakter tes hypostaseos , Ebr. 1:3). Muunganiko wa doxa na hypostasis katika sifa za kiontolojia za Yesu unafafanua hadhi ya Yesu kwa uwazi. Yesu ni utukufu wa Mungu, nafsi ya Mungu. Wimbo (ungamo) huu ulifanyika sehemu ya mkakati wa mwandishi kutofautisha kati ya Yesu na malaika, kama katena ya maandiko ya Agano la Kale na midrash endelevu kwenye maandiko haya inavyothibitisha (ona Ebr. 1:5 2:18). Umbo la uwili na maudhui ya wimbo/maungamo haya—mkazo wake juu ya Yesu na Mungu na Yesu kama Mungu—unapunguza mkanganyiko unaoweza kutokea kati ya Yesu na malaika wenye nguvu. Yesu ni mkuu kiontolojia kuliko mawakala wote wa kimalaika; Yesu ni sawa na Mungu; Yesu ni Mungu. Nguvu ya utendaji ya kuuimba wimbo huu (au kukariri, ikiwa ni kukiri) ilikuwa ni kuimarisha utambulisho wa pamoja kama jamii ya waaminio. Si kwamba ilikuwa na nguvu kidogo kuliko Meza ya Bwana au ubatizo, desturi ya kukiri “Yesu kama utukufu wa Yahwe” iliunda na kuimarisha mipaka kati ya Ukristo na Uyahudi. ~ R. P. Martin and P. H. Davids. Dictionary of the Later New Testament and Its Developments. (electronic ed.). Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 2000.
1
Made with FlippingBook - Online magazine maker