Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook
3 8 /
M U N G U M W A N A
MUUNGANIKO
Somo hili linalenga juu ya Yesu, Masihi na Bwana wa wote, katika suala la uhalali na umuhimuwa kujifunza kwa habari ya nafsi na kazi yaKristo kamaMwokozi, na, hasa katika somo hili, kuwepo kwake kabla kama Neno la Mungu. Ufunuo wa kwamba Yesu, nafsi ya pili ya Utatu, Mungu Mwana, alikuja duniani kwa ajili ya kuufunua utukufu wa Mungu na kuwakomboa wanadamu ni mojawapo ya mafunuo ya kina zaidi ya Maandiko. Kumjifunza Kristo si tu kwa ajili ya udadisi wetu wa kiakili au masomo yetu ya ziada katika elimu ya dini; badala yake ni moyo na nafsi, yaani ndicho kiini chenyewe cha mantiki ya kuwa mfuasi wa Kristo, kuthibitisha katika maisha yetu kwamba hatuwezi kumjua Mungu isipokuwa kupitia mpatanishi wa chaguo lake mwenyewe, Bwana Yesu Kristo. “Alikuja” ni ukiri wa msingi wa jamii ya Wakristo. Bwana yule yule aliyekaa katika fahari na utukufu wa milele pamoja na Baba alifunuliwa kwetu katika mwili kwa njia ya Umwilisho. Tunapotafakari juu ya ukweli huu uliotukuka, tunaongozwa sio tu kustaajabia undani wake, bali kumwabudu na kumwadhimisha Yule ambaye kwa unyenyekevu mkubwa namna hii alikuja duniani ili atukomboe kutoka katika udhalimu wa dhambi. Zilizopo hapa chini ni baadhi ya kweli kuu za kitheolojia zilizofunuliwa katika somo hili. ³ Kanuni ya Imani ya Nikea ina umuhimu mkubwa kwetu tunapochunguza kile ambacho Maandiko yanafundisha kuhusu Kristo, kwa lugha rasmi “Kristolojia.” ³ Fundisho la Kristolojia lina umuhimu mkubwa katika mafunzo yetu kama viongozi katika Kanisa, hasa katika jinsi linavyosaidia kuweka msingi thabiti wa uelewa wetu wote wa hadithi na imani ya Kikristo. ³ Kanuni ya Imani ya Nikea inatengeneza fikra zetu kuhusiana na Yesu na kazi yake, hasa katika namna inavyounda mtazamo wetu kwa habari ya kazi ya Kristo kama mitazamo miwili inayohusiana: kunyenyekezwa kwake (yaani, kufanyika kwake mwanadamu na kufa msalabani kwa ajili yetu) na kuinuliwa kwake (kufufuka kwake, kupaa kwake, na tumaini la kurudi kwake katika nguvu). ³ Elimu mpya ya Kristolojia inaweza kuwawezesha watenda kazi na wahudumu Wakristo wa mijini kudhihirisha vyema zaidi upendo wa Mungu kwa wanadamu, na kutoa ushahidi wa kuvutia zaidi kuhusu ahadi yake tukufu ya Ufalme. ³ Maandiko Matakatifu yanafundisha kwa uwazi kwamba Yesu wa Nazareti, kabla ya kuja duniani, alikuwepo kama mshiriki wa Uungu, Neno Aliyekuwepo hapo awali au Logos . Mafundisho haya ya kibiblia yanathibitishwa kwa moyo wote katika Imani ya Nikea, imani kuu ya awali
Muhtasari wa Dhana Muhimu
1
Made with FlippingBook - Online magazine maker