Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook
/ 3 9
M U N G U M W A N A
ya kiekumene (ya kiulimwengu) inayokiri kuwepo kwa Yesu Kristo kabla ya kuja duniani, na uungu wake. ³ Kuwepo kwa Yesu kabla kumewekwa katika njia tatu zinazohusiana na muhimu katika Maandiko: kwanza kama Mungu Mwana, mtu wa kiungu sawa na Mungu, kama Aliyetarajiwa katika unabii wa Agano la Kale kuhusu Masihi, na pia Neno la Mungu aliyefanyika mwili, Mungu katika umbo la mwanadamu. ³ Wakati ambapoaidha asili yaYesuya kiunguauya kibinadamu inapokataliwa au kueleweka kwa namna potofu na za uongo, mafundisho yanayotokea ni uzushi. Mafundisho mawili ya uzushi mkuu wa kihistoria kuhusu uungu wa Kristo ni Ebionism na Arianism , ambayo yote yanapotosha fundisho la Biblia kuhusu Yesu kama Mwana wa Mungu. ³ Kuelewa, kuthibitisha, na kuadhimisha uungu wa Yesu ni kiini cha ibada na ufuasi wetu unaoendelea. Kukiri ukweli kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu kunaendelea kuwa muhimu kwa kila nyanja ya Imani na ushuhuda wetu kwa ulimwengu. Sasa ni wakati wa kujadili pamoja na wanafunzi wenzako maswali yako kuhusu elimu ya Kristo na dhana ya Mwana wa Mungu aliyekuwepo kabla ya kuja duniani kwa njia ya Umwilisho. Ingawa hatuwezi kupata undani wa mafundisho haya muhimu juu ya uungu na uwepo wa Yesu Kristo, ni muhimu sana sisi kama viongozi tutafute kufanya hivyo. Tukiwa waabuduwaMungu namashahidi wa Injili, ni lazima tujitahidi daima kutafakari na kufahamu ukweli kuhusu Yesu kama Mwana wa Mungu na Masihi. Hakuna kweli utakazokutana nazo kama kiongozi wa Kikristo zitakazoweza kukuimarisha, kukuwezesha, na kukuelekeza zaidi ya zile zinazohusiana na Bwana na Mwokozi wako Yesu Kristo. Kwa kuzingatia hili, ni muhimu kwetu kuelewa vipengele vya uungu wa Kristo, na kutumia ujuzi huo katika ufuasi wetu ndani yake. Je, una maswali gani hasa kuhusiana na maarifa ambayo umejifunza hivi punde? Yawezekana baadhi ya maswali yaliyopo hapa chini yanaweza kukusaidia kuunda maswali yako mwenyewe, mahususi na muhimu zaidi. * Kama kiongozi wa kiroho, kwa nini kujifunza kwako mafundisho kuhusu Kristo kunaweza kuwa muhimu sana katikamaandalizi yako yanayoendelea kwa ajili ya huduma? Elezea. * Ni kwa njia zipi mielekeo ya sasa katika kuhubiri na kufundisha inaondoka au kuelekea kwenye “mlo” unaozingatia zaidi fundisho la Neno? Kwa nini
1
Kutendea kazi somo na matokeo yake kwa mwanafunzi
Made with FlippingBook - Online magazine maker