Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook

4 0 /

M U N G U M W A N A

kufundisha fundisho la Kristo ni muhimu sana hasa kwa makanisa yetu ya mijini? * Je, kuna tofauti gani katika huduma ya maeneo ya mijini ikiwa tunashindwa kusisitiza au kuthibitisha uungu wa Kristo? Elezea jibu lako. * Tunamaanisha nini tunaposema kwamba Yesu ni “mwanadamu kamili na Mungu kamili”? * Kuna uhusiano gani kati ya ufahamu thabiti wa uungu wa Kristo na ibada na sifa zetu kwake kama Bwana? Eleza. * Kwa kuzingatia dini nyingi za sasa za Kipindi Kipya [New Age] na mashambulizi ya imani ya Kiislamu, ni jinsi gani tunapaswa kuandaa makusanyiko yetu kwa kuwajenga waamini na wanafunzi wetu katika ujuzi wa Biblia juu ya Kristo? * Kwa maoni yako, je, unaamini kwamba tunawatayarisha vyema wengine katika fundisho la Kristo kwa kujifunza kweli za kibiblia zinazomhusu, au kwa umakini kutambua na kukanusha makosa na uzushi unaohusishwa na Yesu leo? Tetea jibu lako. * Je, ni mahali gani panapo faa zaidi kufundisha wengine mafundisho kuhusu Kristo—kutokea kwenye mimbari, katika semina, Shule ya Jumapili, au mahali penginepo? Ni nani anayewajibika kuufundisha Mwili kweli zinazohusu fundisho la Kristo? * Ni dhana gani, kama ipo, ambayo bado inakusumbua kuelewa na kuelezea kuhusiana na Kristo na kazi yake katika Umwilisho? Je, ni lazima ufanye nini ili upate kufahamu vyema eneo hilo kuhusiana na Kristo? Katika mazungumzo na baadhi ya Mashahidi wa Yehova wa eneo lako kuhusu Kristo, mmoja wa wahudumu hao Shahidi anaeleza kwamba wao hawaamini kwamba Yesu alikuwepo kabla, bali ndiye kiumbe wa kwanza aliyeumbwa na Mungu. Akiendeleza hoja yake zaidi, anaeleza kwamba Yesu wa Nazareti alikuwa hasa hasa malaika Mikaeli kabla ya kutokea kwake duniani na huduma yake katika Israeli. Mtazamo huu kwamba Yesu alikuwa mzaliwa wa kwanza wa uumbaji wa Mungu kwa maana ya kuwa kiumbe wa kwanza wa Mungu ni wazo la zamani, lililozoeleka sana. Ungewaambia nini Mashahidi hao kuhusiana na maoni yao juu ya Mwana wa Mungu? Yeye ni malaika Mikaeli

Kama mngalielewa yaliyoandikwa na manabii, msingekana kwamba Yeye ni Mungu, Mwana wa Pekee, Asiyezaliwa, Mungu Asiyeelezeka. ~ Justin Martyr (c. 160, E) 1.262. David W. Bercot, ed. A Dictionary of Early Christian Beliefs . Peabody, MA: Hendrickson Publishers, 1998. uk. 96.

1

MIFANO

1

Made with FlippingBook - Online magazine maker