Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook
/ 4 1
M U N G U M W A N A
Kristo alikuja juu yake
Ungejibuje ikiwa mtu fulani katika kutetea hoja yake kuhusu nafsi ya Yesu, angemtofautisha Yesu na Kristo. Kwa maneno mengine, angesema kwamba roho ya Kristo , yaani ile nguvu ya upako wa Mungu, ilikuja juu ya mwanadamu Yesu wakati wa ubatizo; Yesu alikuwa mtu mtakatifu tu ambaye Mungu alimchagua na kuweka roho yake juu yake, na kwa sababu hiyo hakuwako pamoja na Baba kabla ya kuwepo kwake kama mwanadamu. Unaweza kuelezeaje uhusiano wa mwanadamu Yesu na utambulisho wa Kristo, Mpakwa-mafuta wa Mungu?
2
1
Mafundisho ni muhimu, lakini sio Jumapili Asubuhi
Makusanyiko mengi leo hayatilii mkazo ufundishaji na mahubiri ya mafundisho ya Biblia (doktrini) kwenye mimbari na madarasa ya Kanisa. Katika jitihada za kuweka msisitizo mkubwa katika kutengeneza mazingira rafiki kwa “watafutaji” (wanaotamani tu kufahamu zaidi kuhusu Imani yetu), uinjilisti wa mtindo wa maisha (yaani kuzungumzia zaidi masuala ya maisha ya kila siku), na kuzingatia kimkakati kutokuwa na mafundisho mengi ya kina ya kibiblia katika huduma zetu; makanisa mengi yamechagua kuweka mafundisho ya kina ya Biblia katika makusanyiko madogo yenye watu wachache (kama ushemasi/jumuiya, ibada za katikati ya wiki n.k) na kutumia mimbari na makusanyiko makubwa kufundisha na kuhubiri “masomo ya kisasa na ya kueleweka.” Kama ungekuwa mchungaji kiongozi wa kanisa linalokua, falsafa yako ingekuwaje kuhusiana na jukumu la kufundisha somo kama fundisho la Kristo (Kristolojia) katika kipindi cha Jumapili asubuhi? Je, unaweza kufundisha elimu hii, na ikiwa ndivyo, kwa jinsi gani? Baada ya kusikia dhima ya kanisa mojawapo la dhehebu fulani ambayo ni “kujitazama kama jumuiya ambayo inajenga msingi wa ibada na kujitolea katika Yesu Kristo na kazi yake,” baadhi ya makanisa katika dhehebu hilo yameanza kukabiliana nalo kuhusu kauli hiyo. Wakilishutumu kusanyiko hilo kuwa kanisa lenye mwelekeo wa “Yesu pekee” (yaani Christomonistic ), wachungaji wengine wanadai kwamba kutilia mkazo zaidi nafsi ya Kristo pekee kunaweza kusababisha kukana Utatu na kupuuziwa kwa mada nyingine muhimu za kitheolojia. Kanisa linalochunguzwa limepinga hoja hizo na kujitetea kwamba wao, bila shaka, wanaamini katika Utatu, na kwamba wanajua kwamba kuna mambo mengine muhimu ya mafundisho. Hata hivyo, kuna makosa kuhusiana na nafsi ya Kristo yanayoenea katika kila eneo lingine la ungamo, mafundisho, na imani. Kwa maneno mengine, ukikosea katika fundisho la Kristo (Kristolojia), huwezi kuwa Yesu Pekee
3
4
Made with FlippingBook - Online magazine maker