Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook
4 2 /
M U N G U M W A N A
sahihi katika kitu kingine chochote. Je, ni msimamo wa kundi lipi katika ya haya mawili unaonekana kukubaliana zaidi na mafundisho ya Maandiko?
Kanuni ya Imani ya Nikea inatoa muhtasari kwa uwazi na kwa ufupi unaotupa ufahamu juu ya Yesu Kristo na kazi yake. Fundisho la Kristo, au “Kristolojia,” linahusisha uchunguzi wa kina wa Maandiko ya Biblia kuhusu Yesu, hasa katika maana ya kutusaidia kuiona kazi ya Kristo katika sura mbili: kunyenyekezwa kwake (yaani, kufanyika kwake mwanadamu na kufa kwake msalabani kwa ajili yetu), na kuinuliwa kwake (kufufuka kwake, kupaa kwake, na tumaini la kurudi kwake katika nguvu). Yesu wa Nazareti ni Mwana wa Mungu, na kabla ya kuja duniani kwa kusudi la kuufunua utukufu wa Mungu na kuukomboa uumbaji, alikuwepo kama Neno au Logos aliyekuwepo tokea awali. Maandiko yanafundisha kwa uwazi kuhusiana na kuwepo kwake kabla, ikijumuisha nafasi yake kama Mungu Mwana, mtu wa kiungu aliye sawa na Mungu, kama Aliyetarajiwa katika unabii wa Kimasihi wa Agano la Kale, na kisha kama Mwenye mwili, Neno la Mungu aliyefanyika mwili, Mungu katika umbo la mwanadamu. Ikiwa utapenda kupata ufahamu wa kina zaidi kuhusu baadhi ya maarifa yaliyomo katika somo hili la Yesu, Masihi na Bwana wa Wote: Alikuja , unaweza kujaribu vitabu vifuatavyo: Dodd, C. H. The Founder of Christianity. New York: Macmillan, 1970. Fredriksen, Paula. From Jesus to Christ: The Origin of the New Testament Images of Jesus. New York: Oxford University press, 1988. Brown, Raymond. Jesus, God and Man: Modern Biblical Reflections. New York, Paulist Press, 1980. Sasa ni wakati wa kuhusianisha theolojia hii ya juu na huduma halisi ya vitendo, ambayo utaifikiria na kuiombea katika wiki hii yote ijayo. Roho Mtakatifu anakudokeza nini hasa kuhusiana na kujitoa kwako mwenyewe kwa Kristo kama Mwana wa Mungu, Bwana wa kiungu, anayestahili ibada na utii wako binafsi? Je, unawezaje kuelezea upokeaji wako na ufahamu wako wa fundisho hili la Yesu kama Logos aliyekuwepo hapo awali? Je, ni kwa njia gani ujuzi wako wa uungu wa Yesu umeathiri huduma unayofanya sasa hivi mjini? Ni hali gani hasa inayokuja akilini unapofikiria kuhusu namna ambavyo mafundisho ya Biblia kuhusu hali ya utukufu mkuu aliyokuwa nayo Kristo tangu awali yanapaswa kuathiri mitazamo, mawazo, na mwenendo wako unapomwabudu na kumtumikia Bwana Yesu mjini?
Marejeo ya Tasnifu ya Somo
1
Nyenzo na Bibliografia
Kuhusianisha somo na huduma
Made with FlippingBook - Online magazine maker