Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook
/ 5 7
M U N G U M W A N A
d. Yesu, mzao wa kabila na familia ya Daudi, Rum. 1:3 (rej. 2 Sam. 7:12-16; Zab. 89:36-37; Isa. 9:6-7; Yer. 23:5-6; Yer. 33:15-17; nk.)
e. Maelezo ya Paulo kuhusu ukoo wa kibinadamu wa Yesu, Gal. 4:4 (cf. nasaba za wanadamu za Mt. 1:1-17 na Luka 3:23-38).
2. Umuhimu wake kitheolojia
a. Yesu alizaliwa na mwanamke akiwa mwanadamu kamili. (1) Mathayo 2:11 (2) Mathayo 12:47 (3) Mathayo 13:55
2
b. Alijiita mtu, Yohana 8:40.
c. Asili ya kimwili ya Yesu ilikuwa kwa kila namna kama ya kwetu wenyewe. (1) Akakua katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu (Lk 2:52). (2) Alikuwa na sura yamwanadamu, mwenyemwili wa kibinadamu (Yoh. 4:9; Luka 24:13; Yoh. 20:15; cf. Ebr. 2:14). (3) Watu wa wakati wake walitambua asili yake ya kibinadamu (1 Yoh. 1:1-3). (4) Alihisi njaa na kiu, na alihitaji chakula na maji kwa ajili ya kujikimu (Mt. 4:2; Marko 11:12; Yoh. 19:28). (5) Alipata uchovu, alihitaji kulala na kupumzika kama sisi (Yoh. 4:6; Mt. 8:24). (6) Aliteseka kimwili na kufa msalabani (Ebr. 2:9).
Made with FlippingBook - Online magazine maker