Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook
5 6 /
M U N G U M W A N A
2. Umuhimu wake kitheolojia
a. Utendaji kazi wa Roho Mtakatifu na uweza wa Mungu ufunikao ulimfanya Mariamu kuchukua mimba ya Yesu: hakuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamume yeyote ambaye angetumika kama mtoaji mbegu kwa ajili ya nafsi ya Yesu .
b. RohoMtakatifu ndiye aliyekuwa sababu hai ya mimba ya Mariamu: hakuna mwanamume wa kibinadamu aliyehusika katika mimba yake ya kipekee .
2
c. Yesu alishiriki asili ya mwanadamu kikamilifu, na hakukosa kipengele chochote cha kibinadamu ambacho kinapatikana kwetu sote kama wanadamu.
d. Yesu alitungwa mimba katika tumbo la uzazi la mwanamke, akalelewa na mama wa kibinadamu, na akakua kama wanadamu wengine katika muktadha wa familia na ukuaji wa kibinadamu.
Kama alivyozaliwa na Mariamu katika siku za mwisho, vivyo hivyo pia alitoka kwa Mungu kama Mzaliwa wa Kwanza wa kila kiumbe. ~ Irenaeus (c. 180, E/W), 1.576. Ibid. uk. 101.
B. Ubinadamu Wake: Kristo alizaliwa na Bikira Maria.
1. Ushahidi wa kibiblia
a. Kuzaliwa kwa Masihi katika simulizi ya Luka (Luka 2:4-7)
b. Ahadi ya kinabii kwamba bikira atamzaa Masihi (Isa. 7:14)
c. Mimba ya Mariamu na kuzaliwa kwa Yesu katika Mathayo (Mt. 1:25)
Made with FlippingBook - Online magazine maker