Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook

6 6 /

M U N G U M W A N A

Yesu, Masihi na Bwana wa Wote: Aliishi Sehemu ya 2: Utume wa Kimasihi wa Yesu Kristo

Mchungaji Dkt. Don L. Davis

Mambo matatu muhimu ya maisha ya Yesu yanatusaidia kuelewa maana ya utume wake wa Kimasihi. Yesu ndiye Aliyebatizwa aliyejihusisha na taabu na shida za wenye dhambi aliokuja kuwaokoa. Zaidi ya hayo, Yesu ndiye anayewakilisha Uzinduzi wa Ufalme na ndiye Mtangaza Ufalme wa Mungu, akithibitisha tena haki ya Mungu ya kutawala juu ya uumbaji, akidhihirisha kupitia nafsi yake, miujiza, uponyaji, na kutoa pepo, kama ishara za ujio wa Ufalme duniani kwa njia ya nafsi yake. Yesu pia ndiye Mtumishi wa Yehova aliyetarajiwa ambaye alitangaza Habari Njema kwa maskini, akaonyesha haki katikati ya watu wa Mungu, na hatimaye, akatoa uhai wake kuwa dhabihu mbadala na fidia kwa ajili ya wengi. Lengo letu la sehemu hii, Utume wa Kimasihi wa Yesu Kristo , ni kukuwezesha kuona kwamba: • Yesu wa Nazareti aliingia ulimwenguni kama mtu wa jamii ya Israeli, kama Aliyebatizwa aliyejihusisha na taabu na shida za wenye dhambi ambao alikuja kuwaokoa. • Katika nafsi ya Yesu, Ufalme wa Mungu uliongojewa kwa muda mrefu umedhihirika. Katika nafsi yake, Ufalme wa Mungu umekuja. Kwa hiyo Yesu ndiye Mtangaza Ufalme wa Mungu, akithibitisha tena haki ya Mungu ya kutawala juu ya uumbaji, akidhihirisha kupitia nafsi yake, miujiza, uponyaji, na kutoa pepo, kama ishara za ujio wa Ufalme duniani kwa njia ya nafsi yake. • Katika kutimiza unabii wa Agano la Kale, Yesu ndiye Mtumishi wa Yehova Atesekaye. Tangu tangazo la hadharani la huduma yake ya hadhara na katika nyakati zote za maisha yake, Yesu alijidhihirisha kuwa Mtumishi wa Yehova aliyetarajiwa ambaye angetangaza Habari Njema kwa maskini, kutenda haki katikati ya watu wa Mungu, na hatimaye kutoa uhai wake kuwa dhabihu mbadala kwa ajili ya dhambi za watu.

Muhtasari wa Sehemu ya 2

2

Made with FlippingBook - Online magazine maker