Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook
/ 6 7
M U N G U M W A N A
I. Yesu Ndiye Aliyebatizwa Aliyejihusisha na Wenye dhambi.
Muhtasari wa Sehemu ya 2 ya Video
A. Picha ya kibiblia ya Yesu kama Aliyebatizwa
Tunamwimbia Aliye Juu Sana pekee na Mwanawe wa Pekee, ambaye ni Neno na Mungu. ~ Origen (c. 248, E), 4.639. David W. Bercot, ed. A Dictionary of Early Beliefs . Peabody, MA: Hendrickson Publishers, 1998. uk. 99.
1. Yohana Mbatizaji (cf. Mt. 3:1-12; Mk. 1:2-8; Lk 3:1-20; Yoh. 1:19-28)
2. Yohana kama mtangulizi wa Masihi katika unabii wa AK
a. Yeye ndiye mjumbe anayetengeneza njia mbele ya Masihi (Mal. 3:1).
2
b. Yeye ndiye sauti ya mtu aliaye nyikani (rej. Isa. 40:1-3 na Mt. 3:1-3).
c. Alitabiriwa kuwafundisha watu njia za Bwana (Mal. 2:7).
d. Alikuja katika roho ya Eliya na nguvu zake. (1) Malaki 4:5-6 (2) Mathayo 11:13-14
e. Unabii ulitolewa kuhusu maisha na utume wa Yohana kabla ya Masihi kutokea (rej. Luka 1:13-17).
3. Yesu anamkubali Yohana kama mjumbe mtangulizi wa Masihi (Mt.11:10-11).
Made with FlippingBook - Online magazine maker