Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook

7 6 /

M U N G U M W A N A

³ Maandiko yanafundisha kwa hakika kwamba Yesu wa Nazareti ni mwanadamu kamili, ambaye alichukuliwa mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu na kuzaliwa na mwanamke, Bikira Maria. ³ Mafundisho mawili mashuhuri ya uzushi ya kihistoria ambayo yalipinga ubinadamu wa Yesu yaliwekwa wazi na kukanushwa katika mabaraza ya Kanisa la kwanza. Unestoria ( Nestorianism ), fundisho kwamba Kristo alikuwa nafsi mbili tofauti, na Ueutikia (Eutychianism), fundisho kwamba Kristo ana asili moja iliyochanganyika, yalikataliwa na kupingwa vikali kuwa ni uzushi kwa sababu yaliukataa ubinadamu kamili wa Yesu. Mabaraza ya Nikea (325) na Chalcedon (381) yalisuluhisha mkanganyiko huu, yakithibitisha kwamba Yesu alikuwa Mungu kamili na mwanadamu kamili. ³ Mabaraza ya awali pia yalikanusha na kupinga makosa mengine makubwa yanayohusiana na kutafsiri vibaya ubinadamu wa Yesu: Docetism ambayo ilidai kwamba Yesu hakuwa mwanadamu na Apollinarianism ambayo ilidai kwamba Yesu hakuwa mwanadamu kamili. ³ Mafundisho ya ubinadamu wa Kristo yamejaa athari nyingi na muhimu za kiutendaji za umoja wa asili ya Yesu ya uungu na ya ubinadamu. Yesu akiwa kama sisi katika kila namna lakini bila dhambi na akiwa Kuhani Mkuu wetu, anaweza kuelewa mahitaji yetu na kutuwakilisha mbele za Mungu. Kama Adamu wetu wa Pili; tutafananishwa na mwili wake wa utukufu katika wakati wa utukufu ujao. ³ Yesu wa Nazareti aliingia ulimwenguni kama mtu wa jamii ya Israeli, kama Aliyebatizwa ambaye alijihusisha na taabu na shida za wenye dhambi aliokuja kuwaokoa. ³ Kupitia nafsi ya Yesu, Ufalme wa Mungu uliongojewa kwa muda mrefu umedhihirika. Katika nafsi yake, Ufalme wa Mungu umekuja. Kwa hiyo Yesu ndiye Mtangaza Ufalme wa Mungu, akithibitisha tena haki ya Mungu ya kutawala juu ya uumbaji, akidhihirisha kupitia nafsi yake, miujiza, uponyaji, na kutoa pepo, kama ishara za ujio wa Ufalme duniani kwa njia ya nafsi yake. ³ Katika kutimiza unabii wa Agano la Kale, Yesu ndiye Mtumishi wa Yehova Atesekaye. Tangu tangazo la hadharani la huduma yake ya hadhara na katika nyakati zote za maisha yake, Yesu alijidhihirisha kuwa Mtumishi wa Yehova aliyetarajiwa ambaye angetangaza Habari Njema kwa maskini, kutenda haki katikati ya watu wa Mungu, na hatimaye kutoa uhai wake kuwa dhabihu mbadala (fidia) kwa ajili ya dhambi za watu.

2

Made with FlippingBook - Online magazine maker