Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook
/ 7 7
M U N G U M W A N A
Sasa ni wakati wa kujadiliana pamoja na wanafunzi wenzako maswali yako binafsi kuhusu Yesu na kazi yake kama Masihi aliyeishi kati yetu. Uwezo wako wa kuwafanya wengine kuwa wanafunzi wa Yesu unategemea moja kwa moja ufahamu wako wa Yeye alikuwa nani, alifanya nini (na kwa nini), na namna yale aliyofanya (na anayofanya) yanavyohusiana na maisha yako na huduma yako pia. Unapotafakari baadhi ya kweli zilizofundishwa katika somo hili, ni aina gani ya masuala na mawazo yamejitokeza ambayo wewe binafsi unahitaji majibu yake? Ni masuala gani yamefunuliwa kupitia somo hili ambayo yanaathiri ufuasi wako binafsi na kutembea kwako na Bwana? Maswali yaliyopo hapa chini yameundwa ili kukusaidia kuunda maswali yako mwenyewe, mahususi na ya kipekee zaidi. * Inawezekanaje kwamba Mungu angeweza kuwa mwanadamu kwa kusudi la ufunuo na ukombozi? Je, ni muhimu kwetu kuelewa namna hili linavyowezekana, au tunapaswa kuzingatia tu kwamba lilitokea? Elezea jibu lako. * Ni kwa kiwango gani nadharia kuhusu namna asili ya Yesu ya kiungu na ya kibinadamu zilivyounganishwa hatimaye ni suala la fumbo (siri) na la imani, na si la kiakili na kiuchambuzi? Elezea jibu lako. * Je, ni sawa kusema kwamba Yesu kwa kila namna alikuwa kama sisi isipokuwa hakutenda dhambi kamwe? Kwa maneno mengine, je, kwa kila namna Yesu alikuwa kama sisi katika mihemko, mawazo yake, hisia zake za kibinadamu na mahitaji yake? * Je, ni kwa njia gani makosa (yaani, mafundisho ya uzushi ya kale) kuhusu ubinadamu wa Yesu yanajitokeza katika dhana potofu kuhusu Yesu leo? Ni kwa jinsi gani mawazo ambayo watu wanayo kuhusu Yesu leo ​yanafanana na yale ambayo yalikanushwa katika Mabaraza Makuu ya Kanisa? * Kwa nini ni muhimu sana kuweza kuwaambia wengine kwamba Yesu anajali na anaelewa udhaifu wetu? Ni kwa jinsi gani fundisho la ubinadamu wake linatusaidia kueleza na kuwasilisha ukweli huu kuhusu kujali kwa Yesu kwa wale tunaowatumikia mijini? * Sisi kama wahudumu katika maeneo ya mijini tunapaswa kuutangazaje Ufalme wa Mungu kwa kuwaaminisha watu kwamba Ufalme upo jijini leo? Ni katika maana gani mahubiri na mafundisho yetu ni lazima yakazie pande zote mbili za mtazamo wa Kristo kuzindua Ufalme katika ujio wake wa kwanza, na kuukamilisha katika Kuja kwake Mara ya Pili? * Agano Jipya linathibitisha kwamba nia ya Mungu ni kwamba sisi kama watu wake tufanane na mfano wake, katika kifo chake na vilevile katika
Kutendea kazi somo na matokeo yake kwa mwanafunzi
2
Made with FlippingBook - Online magazine maker