Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook

8 0 /

M U N G U M W A N A

Yesu alikuja duniani kama mwanadamu ili kutufunulia sisi wanadamu utukufu wa Baba na kutukomboa kutoka katika dhambi na nguvu za Shetani. Yesu alikuwa mwanadamu kamili, alichukuliwa mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu na kubebwa hadi kuzaliwa na Bikira Maria. Mafundisho mawili ya kizushi ya kale yalipinga dhana ya Yesu kufanyika mwanadamu: Unestoria (Nestorianism) – kwamba Kristo alikuwa watu wawili tofauti , na Ueutikia (Eutychianism) – kwamba Kristo ana asili moja iliyochanganyika . Mitaguso ya Nikea (325) na Chalcedon (381) ilisuluhisha maswali haya, ikithibitisha kwamba Yesu alikuwa Mungu kamili na mwanadamu kamili . Mafundisho mengine ya uzushi yaliyotafsiri vibaya maana ya ubinadamu wa Yesu: Docetism, ambayo ilidai kwamba Yesu hakuwa mwanadamu na Uapolinari (Apollinarianism) ambao ulidai kwamba Yesu hakuwa mwanadamu kamili . Yesu, hata hivyo, ni mwanadamu kamili na anaweza kutuwakilisha kikamilifu mbele za Mungu kama kuhani wetu mkuu, mpatanishi wetu, na kielelezo kipya cha ubinadamu uliotukuzwa kama Adamu wetu wa Pili. Mambo matatu muhimu katika maisha ya Yesu yanatusaidia kuelewa maana ya utume wake wa Kimasihi. Yesu ndiye Aliyebatizwa aliyejihusisha na taabu na shida za wenye dhambi ambao alikuja kuwaokoa. Zaidi ya hayo, Yesu ndiye anayewakilisha Uzinduzi wa Ufalme wa Mungu na ndiye Mtangaza Ufalme wa Mungu, akithibitisha tena haki ya Mungu ya kutawala juu ya uumbaji wote, akidhihirisha kupitia nafsi yake, miujiza, uponyaji, na kutoa pepo kama ishara za ujio wa Ufalme duniani kwa njia ya nafsi yake. Yesu pia ndiye Mtumishi wa Yehova aliyetarajiwa ambaye alitangaza Habari Njema kwa maskini, akaonyesha haki katikati ya watu wa Mungu, na hatimaye, akatoa uhai wake kuwa dhabihu mbadala na fidia kwa ajili ya wengi. Ikiwa utapenda kupata ufahamu wa kina zaidi kuhusu baadhi ya maarifa yaliyomo katika somo hili liitwalo Yesu, Masihi na Bwana wa Wote: Aliishi , unaweza kujaribu vitabu vifuatavyo: Brown, Raymond E. The Birth of the Messiah . New York: Doubleday, 1979. Hoehner, Harold W. Chronological Aspects of the Life of Christ. Grand Rapids: Zondervan, 1977. Ladd, George Eldon. Jesus and the Kingdom. New York: Harper, 1964. Meier, John P. A Marginal Jew: Rethinking the Historical Jesus . New York: Doubleday, 1991.

Marejeo ya Tasnifu ya Somo

2

Nyenzo na Bibliografia

Made with FlippingBook - Online magazine maker