Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook
/ 8 1
M U N G U M W A N A
Katika kuangazia eneo kubwa la kitheolojia katika somo letu, ni lazima tuchukuemuda wa kutulia na kutafakari ili kuona theolojia hii ya juu ina uhusiano gani na maisha yetu na shughuli zetu katika huduma. Ubinadamu na maisha ya Bwana wetu yanagusa masuala kadhaa ya kivitendo katika maisha yetu ambayo tunahitaji kushughulikia. Ni maswali gani hasa ambayo Roho Mtakatifu amekuwa akiyaleta kwako kuhusu ufahamu wako wa maisha ya Yesu, na jinsi unavyoishi kwa kufuata kielelezo cha maisha yake leo? Je, kuna wazo fulani ambalo Bwana amekupa kuhusu maisha na huduma yakomwenyewe ambalo unahitaji kutendea kazi wiki hii kuhusiana na kanuni ambazo umejifunza hapa? Je, kuna hali fulani ambayo inakuja akilini unapofikiria njia mahususi ambayoMungu pengine anataka kulifanya fundisho hili lipate nafasi, nguvu na ushawishi katika namna unavyotembea na Yeye, mahusiano yako na wengine, au katika mafundisho na ushauri wako kwa wanafunzi wa Kristo unaowalea? Yapeleke haya yote mbele za Mungu katika maombi, ukimwomba hekima na msaada wake unapochunguza uhusiano wa kweli hizi na hali yako ya maisha leo. Kama ilivyo katika kila somo, ni muhimu sana tuwaombe kaka na dada zetu, na viongozi wetu watuombee ili tuweze kuzitafakari na kuzitumia kwa ufasaha na ufanisi kweli za Neno la Mungu. Kweli ya Mungu kuhusu fundisho la Kristo (Kristolojia) ni kwa ajili ya kutujenga na kutubadilisha , si tu kwa ajili ya udadisi na tafakuri yetu . Maombi huuisha kweli ndani yetu katika namna ambayo masomo peke yake hayawezi kufanya. Mwombe mshauri na/au mwalimu wako akuombee ili uweze kutendea kazi, kuwashirikisha wengine, na kufundisha na kuhubiri kweli hizi kwa namna bora na mpya katika Kanisa na huduma yako. Mwombe Roho Mtakatifu akuwezeshe kufahamu upya na kuitumia nguvu ya uzima ya fundisho la Kristo – maisha yake yasiyo na kifani na huduma yake ya kweli – kwa wengine. Mwombe Mungu akupe hekima unapotafuta kufanya fundisho hili liwe hai, katika maisha yako mwenyewe na ya wengine. Tuwe na uhakika kwamba atatupatia hekima ikiwa tu tutaamini (Yakobo 1:5).
Kuhusianisha somo na huduma
2
Ushauri na maombi
MAZOEZI
Waebrania 2:14-17
Kukariri Maandiko
Ili kujiandaa kwa ajili ya kipindi, tafadhali tembelea www.tumi.org/books kupata kazi ya usomaji ya wiki ijayo, au muulize Mkufunzi wako.
Kazi ya usomaji
Tafadhali soma kwa umakini kazi zilizo hapo juu na kama wiki iliyopita, ziandikie muhtasari mfupi na ulete muhtasari huo darasani wiki ijayo (tafadhali angalia
Kazi Nyingine
Made with FlippingBook - Online magazine maker