Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook

9 0 /

M U N G U M W A N A

Yesu, Masihi na Bwana wa Wote: Alikufa Sehemu ya 1: Kunyenyekezwa na Kifo chake

YALIYOMO

Mchungaji Dkt. Don L. Davis

Kunyenyekezwa kwa Yesu Kristo, tukitumia maneno ya mwanatheolojia Oden, kunahusu kushuka kwake kutoka mbinguni akiuacha utukufu wake wa kiungu, kuja duniani na kufa kwa ajili ya ulimwengu. Unyenyekevu huu uliakisiwa katika kila nyanja ya Umwilisho wa Yesu na maisha yake duniani, tangu kuzaliwa kwake hadi maisha na huduma yake. Kilele cha kushuka na kunyenyekea huku kinadhihirishwa katika mateso na kifo chake pale Kalvari. Kifo chake kinaweza kueleweka kupitia vipengele mbalimbali vinavyotuwezesha kuelewa vizuri zaidi asili ya wokovu wetu ndani yake: kifo chake kilikuwa fidia kwa ajili yetu, upatanisho wa dhambi zetu, dhabihu mbadala badala yetu, ushindi dhidi ya shetani na kifo chenyewe, na upatanisho kati ya Mungu na wanadamu. Lengo letu katika sehemu hii, Kunyenyekezwa na Kifo chake , ni kukuwezesha kuona kwamba: • Kunyenyekezwa kwa Yesu Kristo kunawakilishwa na kushuka kwake kutoka katika makao ya mbinguni katika utukufu wake kuja duniani kuteseka na kufa kwa ajili ya ulimwengu. • Yesu alidhihirisha unyenyekevu na kujishusha kwake katika kila hali ya Umwilisho wake, katika kuzaliwa kwake na katika maisha yake yote na huduma yake. • Kilele cha kushuka na kunyenyekea huku kinadhihirishwa katika mateso na kifo cha Yesu Kristo. • Kifo cha Yesu kinaweza kueleweka kupitia vipengele mbalimbali vinavyotuwezesha kuelewa mbaraka ambao mateso yake yaliutoa kwa ulimwengu. Vipengele hivi ni pamoja na dhana ya kifo cha Yesu kama fidia kwa ajili yetu, kama upatanisho kwa ajili ya dhambi zetu, kama dhabihu mbadala badala yetu, kama ushindi dhidi ya ibilisi na kifo chenyewe, na kama upatanisho kati ya Mungu na wanadamu. • Kanuni ya Imani ya Nikea inakiri wazi wazi kwamba Bwana wetu Yesu Kristo alikufa na akazikwa kwa ajili ya dhambi zetu. Huu ulikuwa mwisho na kilele cha kunyenyekezwa kwa Bwana wetu duniani katika kushuka kwake kutoka mbinguni, akiuacha utukufu wake wa kimbingu aliokuwa nao hapo awali.

Muhtasari wa Sehemu ya 1

3

Made with FlippingBook - Online magazine maker