Mungu Mwana, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 10 Swahili Student Workbook
/ 9 1
M U N G U M W A N A
I. Kunyenyekezwa kwa Yesu Kristo
Muhtasari wa Sehemu ya 1 ya Video
Wafilipi 2:6-8 -. . . ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; 7 bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; 8 tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba. Wagalatia 4:4-5 - Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria, 5 kusudi awakomboe hao waliokuwa chini ya sheria, ili sisi tupate kupokea hali ya kuwa wana.
Kwa njia ya mti tulifanywa kuwa
wadeni kwa Mungu. Vivyo hivyo, kwa njia ya mti [msalaba], tunaweza kupata ondoleo la deni letu. ~ Irenaeus (c. 180, E/W), 1.545. David W. Bercot, ed. A Dictionary of Early Christian Beliefs . Peabody, MA: Hendrickson Publishers, 1998. uk. 184.
A. Kunyenyekezwa katika Umwilisho: Yesu Kristo kujifanya kuwa hana utufu
1. Aliacha kule kuwa kwake sawa na Mungu.
3
a. Kukubali kuondoka katika uwepo na ushirika na Baba na Roho.
b. Aina ya roho na utukufu usio na kikomo.
2. Alijifanya si kitu na kuchukua namna ya mtumwa (kwa mfano wa mwanadamu).
a. Alizaliwa na mwanamke katika mazingira duni sana.
b. Alilelewa katika mazingira ya kutokujulikana (hakuna aliyejua yeye ni nani kwa muda mrefu wa maisha yake).
Made with FlippingBook - Online magazine maker