Mungu Roho Mtakatifu, Kitabu cha Mwanafunzi, Capstone Module 14 Swahili Student Workbook

/ 5 7

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

B. Kushughulikia dhana potofu kuhusu unabii

1. Dhana potofu #1: Unabii wote unatabiri wakati ujao.

a. Kwa sehemu unabii unatabiri wakati ujao. Kwa mfano: (1) Onyo la Mungu kuhusu hukumu ijayo juu ya dhambi

(2) Ufunuo endelevu wa unabii kuhusu mpango wa Mungu, hususani mpango wake wa kumleta Masihi (mf. Isa. 11:1; Mik. 5:2)

2

b. Unabii wa utabiri wa wakati ujao unafaida sana, hata hivyo ni sehemu ndogo sana ya jumla ya Neno la kinabii, yaani Maandiko Mtakatifu.

c. Gordon Fee na Douglas Stuart wanasema: “chini ya asilimia 2 ya unabii wa Agano la Kale ni Wakimasihi. Chini ya asilimia 5 unaelezea Agano Jipya. Chini ya asilimia 1 unaelezea matukio ambayo bado hayajatokea.”

d. Kwa sehemukubwaunabii ni ufunuokuhusunafsi yaMungu, kuhusu tabia yake, kuhusu uhusiano wake na watu wake aliowachagua, na kuhusu makusudi yake kwa wanadamu wote badala ya utabiri wa matukio yajayo. Kutofautisha hoja hizi kitheolojia ni kwamba unabii wote unahusu kutabiri (kuwasilisha ujumbe wa Mungu) kwa ajili ya wakati wa sasa (forthtelling) , wakati kwa sehemu unabii unahusisha pia kutabiri matukio ya wakati ujao (foretelling) .

2. Dhana potofu #2: Unabii unapatikana katika sehemu moja tu ya Maandiko.

a. Maandiko ya Kiebrania yalipangwa katika sehemu tatu – Torati au Sheria (Torah) , Manabii (Nevi’im) , na Maandiko (Ketuvim) .

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker