Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide

/ 1 0 1

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

tendo la kuunganishwa na Kristo, kila kitu ambacho Kristo anacho, Mungu anakihesabu kuwa ni cha kwetu.

3. Wakati wa wokovu, (pale tunapoungana na Kristo), tunapewa ukaribu uleule na Roho Mtakatifu kama Yesu alivyo karibu naye. Katika suala la ubatizo katika Roho Mtakatifu, hii ina maana kwamba kwa kuwa Yesu anaye Roho “pasipo kikomo” (Yohana 3:34-35), nasi kadhalika tumepewa Roho huyo katika Kristo. Hoja ya mtazamo huu ni kwamba huwezi kuwa na Roho Mtakatifu zaidi ya unavyompokea wakati wa wokovu kwa sababu katika wokovu unapewa uwezo wa kupokea kila kitu ambacho ni cha Kristo.

ukurasa 256  9

4. Kukua katika Kristo kunahusisha kujifunza jinsi ya kuishi wakati mmoja baada ya mwingine kwa kutegemea nguvu za Roho Mtakatifu ambazo Mungu anatupa pale tunapookoka.

ukurasa 256  10

3

a. Mtazamo huu unasisitiza kwamba waongofu wapya mara nyingi hawatambui kile ambacho wamepewa au kujua jinsi ya kuishi maisha yao mapya katika Roho. Wakati wa wokovu, tunapewa Roho Mtakatifu ambaye anakaa ndani yetu kikamilifu na kututia nguvu na uwezo wote (1 Kor. 6:19), lakini lazima tujifunze “kuenenda katika Roho” (Gal. 5:16-26) kila siku. Kutokana na msimamo wa makanisa ya Reformed, kila mwamini “amebatizwa katika Roho Mtakatifu” lakini si kila mwamini amepevuka ili waweze kutembea katika nguvu na utakatifu ambao ungefanya matokeo ya ubatizo huo kuwa dhahiri. Ukuaji huu katika maisha yaliyojazwa na Roho ni mchakato unaoendelea ambao haukomi. Hata mwamini aliyekomaa zaidi hatapata uhuru kamili kutokana na dhambi na kuweza kutegemea nguvu za Roho kwa asilimia zote, hadi atakapokufa na kutukuzwa. b. Chimbuko katika Maandiko: Theolojia ya mtazamo huu wa makanisa ya Reformed kuhusu ubatizo katika Roho Mtakatifu kwa kiasi kikubwa inatokana na Nyaraka za Paulo. Hadithi za Kitabu cha Matendo ya Mitume lazima zilinganishwe na maelezo ya wazi ya Paulo.

Kwa hakika lingekuwa ni kosa kujaribu kuweka msingi wa fundisho lenye umuhimu wa kitheolojia kiasi hiki juu ya vifungu katika Maandiko ya Luka [Matendo] ambavyo vilikusudiwa kuelezea hatua mbalimbali ambazo zilionekana kwake kuwa muhimu katika kuenea kwa kazi ya Mungu. ~ Michael Green. I Believe in the Holy Spirit . uk. 162.

Made with FlippingBook - Share PDF online