Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide
1 0 2 /
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
5. Muhtasari wa msimamo wa makanisa ya Reformed
ukurasa 257 11
a. Nini maana ya “Ubatizo katika Roho Mtakatifu”? Njia ambayo mtu anaungamanishwa na Kristo na Kanisa lake (1 Kor. 12:7, 13; Efe. 4:4-5; Gal. 3:2).
b. Ni lini mtu anaupokea “Ubatizo wa Roho Mtakatifu”? Wakati tunapookoka – mtu anapotubu na kumwamini Yesu kama Bwana na Mwokozi (Mdo. 2:38-39, Rum. 8:9).
c. Je, “ubatizo wa Roho” unapokelewaje? Kwa imani iokoayo katika Yesu Kristo (Yohana 7:37-39).
3
d. Je, ni ushahidi gani au uthibitisho gani unaonyesha “ubatizo wa Roho” umepokelewa? Kudumu katika imani (Yohana 15:4; Flp. 3:12-14).
e. Je, “ubatizo wa Roho Mtakatifu” unatimiza nini? Unatufanya kuendelea zaidi kuwa kama Yesu Kristo (2 Kor. 3:18; Yoh. 15:4, Rum. 12:1-2).
C. Mtazamo wa Ubatizo wa Roho kama tendo lenye hatua nyingi
1. Mtazamo wa hatua nyingi unaamini kwamba Roho hutolewa wakati wa wokovu lakini pia kwamba utimilifu mkubwa zaidi wa Roho hupokelewa baadaye, jambo ambalo humwezesha mtu kushuhudia utendaji wa Roho kwa ukamilifu zaidi katika maisha na huduma yake.
Made with FlippingBook - Share PDF online