Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide
/ 1 0 3
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
2. Wale wanaoamini kwamba Roho Mtakatifu huja juu ya watu katika hatua mbili au zaidi wana mitazamo tofauti kuhusu kusudi la ujio huu lakini wote wanatumia Maandiko yale yale kuunga mkono wazo kuu kwamba kuna kazi ya pili ambayo Roho Mtakatifu anafanya ndani ya watu baada ya wokovu. Vifuatavyo ni baadhi ya vifungu muhimu vya Maandiko ambavyo vinatumika. a. Umisheni wa Filipo kwenda Samaria (Matendo 8) Filipo anawabatiza watu kama wakristo wapya lakini wanapokea “ujazo” wa Roho Mtakatifu baada tu ya Petro na Yohana kuja na kuwawekea mikono. b. Paulo kwenye nyumba ya Anania (Matendo 9) Paulo anaongoka akiwa njiani kuelekea Dameski na kupokea utume wake wa utumishi wa kimishenari (taz. Mdo 26:13-19), lakini anajazwa na Roho Mtakatifu baada tu ya Anania kumwekea mikono. c. Wanafunzi wa Yohana Mbatizaji wanabatizwa na Paulo katika jina la Yesu (Mdo 19). Wanafunzi waliobatizwa na Yohana Mbatizaji walijua kwamba Yesu alikuwa Masihi lakini hawakuwa wamefundishwa vya kutosha kuhusu Roho Mtakatifu. Paulo anawauliza, “Je, mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini?” Wale wanaoamini katika Ubatizo wa Roho kama tendo lenye hatua nyingi wanasema kwamba swali hili halileti mantiki yoyote isipokuwa kama kuna tendo maalum linalofanywa na Roho Mtakatifu ambalo ni tofauti na tendo la kukoka. d. Matukio ya Mitume wa Yesu (1) Katika Yohana 20:22 – Yesu anawapulizia mitume na wanapokea Roho Mtakatifu, lakini katika Matendo ya Mitume 1:4-8, anawaagiza mitume hao hao wangojee Yerusalemu kuja kwa Roho Mtakatifu ili wapokee nguvu ya kuwa mashahidi.
3
Made with FlippingBook - Share PDF online