Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide
/ 1 1 7
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
Uwepo Wenye Nguvu wa Roho Mtakatifu Sehemu ya Pili
S O M O L A 4
ukurasa 261 1
Karibu katika Jina lenye nguvu la Yesu Kristo! Baada ya kusoma, kujifunza, kufanya majadiliano na kutendea kazi yote yaliyomo katika somo hili, utakuwa na uwezo wa kufanya yafuatayo: • Kutumia akrostiki ya RABBIS ili kukumbuka kazi ya Roho Mtakatifu katika maisha ya mwamini. • Kuelezea maana na umuhimu wa kitheolojia wa jukumu la Roho la kutoa karama, kukaa ndani ya mwamini, kutia muhuri, na kuwatakasa waamini katika Kristo. • Kutambua Maandiko ya msingi yanayoonyesha kwamba Mungu anatoa karama, anakaa ndani ya mwamini na kuwatakasa waaminio katika Kristo kupitia kazi ya Roho Mtakatifu. Soma Warumi 8:26. Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa. [Soma makala ya ibada yenye kichwa “The Spirit Himself ” kutoka kwenye kitabu kiitwacho Names of the Holy Spirit, kurasa za 138-140.] Baada ya kutamka/kuimba Kanuni ya Imani ya Nikea (katika kiambatisho) sali sala ifuatayo: Pulizia pumzi yako ndani yangu Roho Mtakatifu, ili nia yangu igeukie mambo matakatifu. Nitie nguvu, Roho Mtakatifu, ili niweze kuutunza utakatifu huo. Nilinde, Roho Mtakatifu, ili kamwe nisiupoteze utakatifu nilioupokea. Amina. ~ Mtakatifu Augustine, Askofu wa Hippo na mmoja wa wanatheolojia muhimu sana wa Kanisa. Aliishi miaka ya 354B.K hadi 410B.K. William Lane, S.J. Praying with the Saints. Dublin, Ireland: Veritas, 1989. uk. 20. Roho Mwenyewe
Malengo ya Somo
Ibada
4
Kanuni ya Imani ya Nikea na Sala
Made with FlippingBook - Share PDF online