Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide

1 1 8 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

Weka kando madokezo yako, kusanya mawazo na tafakari zako, na ujibu maswali ya jaribio la Somo la 3, Uwepo Wenye Nguvu wa Roho Mtakatifu (Sehemu ya Kwanza).

Jaribio

Fanya mazoezi pamoja na mwanafunzi mwenzako, andika na/au nukuu kwa kutamka andiko la kukumbuka kutoka kwenye andiko la kipindi kilichopita: Warumi 8:22-25.

Mazoezi ya Kukariri Maandiko

Kusanya muhtasari wako wa kazi ya usomaji ya wiki iliyopita, yaani, jibu lako lenye maelezo machache kuhusu mambo muhimu uliyoyaona katika vitabu ulivyoelekezwa kusoma, yaani hoja kuu ambazo waandishi walitaka kuziwasilisha (taz. Fomu ya Ripoti ya Usomaji).

Kazi za kukusanya

MIFANO YA REJEA

Mjadala: Karama za Rohoni

Katika Kitabu chao kiitwacho Soar With Your Strengths, waandishi Donald Clifton na Paula Nelson wanasimulia mfano kuhusu shule iliyokuwa ikiendeshwa kwa ajili ya wanyama katika bustani ya malisho. Waalimu katika shule ile waliamini kwamba mnyama ambaye wangempa mafunzo vizuri angeweza kukimbia, kuogelea, kukwea juu ya miti, kuruka, na kupaa. Sungura alipoingia shuleni hapo, kila mtu alijua kitakachotokea: alifanya vizuri sana katika kukimbia na kuruka lakini hakuweza kabisa kuogelea, kukwea juu ya miti, na kupaa. Waalimu wake wakaamua kumshauri atumie muda mrefu zaidi katika kujinoa na kuboresha yale maeneo ambayo hakuweza kufanya vizuri. Hivyo sungura ambaye zamani alikuwa anatumia siku muda wake mwingi kukimbia na kuruka, akawa sasa akitumia muda mwingi akijitahidi kujifunza kuogelea na kupaa na akajikuta mara kwa mara akiishia kudharauliwa au kupata majeraha. Matokeo yake, akaichukia kabisa shule. Mwishoni mwa mfano ule, hata hivyo, akashauriwa na bundi mzee mwenye hekima kwamba ni busara kuwa na maono ya ulimwengu ambamo kila mtu anafanya mambo yaliyo ndani ya uwezo, vipawa, na ujuzi wake kuliko kujaribu kuwa vile ambavyo kamwe haukukusudiwa kuwa. Katika 1 Wakorintho 12 Mtume Paulo anatoa mfano wa aina hiyo hiyo lakini badala ya kutumia wanyama yeye anatumia sitiari ya mwili wa mwanadamu. Macho yanaona vizuri lakini hayasikii. Masikio yanasikia vizuri lakini hayana uwezo wa kunusa. Jibu ambalo Paulo anatoa kuhusiana na fumbo hili ni kutokujaribu kulazimisha kila kiungo cha mwili kifanye kila kitu vizuri, lakini badala yake watu watiwe moyo kufanya kazi pamoja ili kwamba kila mmoja atumie karama aliyopewa na Roho Mtakatifu kwa ajili ya manufaa ya mwili wote.

1

4

Made with FlippingBook - Share PDF online