Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide

1 2 4 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

Kwa kuzingatia hili, uhalali wa karama yoyote ya rohoni unathibitishwa kwa nama karama husika inavyoakisi kwa uaminifu kweli muhimu za Maandiko (1Thes. 5:21; Yuda 3), kwa uwezo wake wa kuujenga mwili wa Kristo (1Kor. 14:12), na namna inavyotumika kwa kuongozwa na upendo wa kweli kwa Mungu na kwa wengine (rej. 1Kor. 13), katika unyenyekevu kwa mamlaka halali ya kanisa (Ebr. 13:17). ~ Mch. Terry G. Cornett

3. Karama zinazoelezewa katika Agano Jipya

ukurasa 266  6

a. Kwa maelezo ya karama hizi, tazama: (1) “Jedwali la Karama za Rohoni Zilizotajwa Kimahususi katika Agano Jipya” (tafadhali rejelea kwenye Viambatisho vya Kitabu hiki). (2) Craig S. Keener, Gift and Giver, kurasa za. 113-136 (maelezo ya kozi). b. Kuainisha karama katika makundi Jambo moja ambalo watu wengi wanaona kuwa linafaa ni kupanga karama za rohoni katika makundi ambayo yanaonyesha kile ambacho Mungu anafanya kupitia kila karama husika. Wanatheolojia kwa miaka mingi wamekuwa na njia nyingi tofauti za upangaji huu lakini namna moja ninayoona inasaidia sana ni kuziainisha katika makundi ya karama za neno, karama za huduma, karama za nguvu, na karama za uongozi. (1) Karama za Neno (a) H izi ni karama ambazo zinafanya nia ya Mungu ijulikane. (b) K arama hizi zinajumuisha kupambanua roho, uinjilisti, kuonya, maarifa, unabii, ualimu, na hekima. (c)  Karama hizi zinapotenda kazi katika Kanisa, watu wa

4

Mungu wanaelewa vyema zaidi mipango ya Mungu, maadili ya Mungu, utume wa Mungu, na amri za Mungu na wanaweza kuona kwa uwazi zaidi jinsi ya kuzitii.

Made with FlippingBook - Share PDF online