Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide
/ 1 2 5
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
(2) Karama za Huduma (a) H izi ni karama ambazo zinaudhihirisha moyo wa Mungu. (b) K arama hizi zinajumuisha utowashi (ambao unampa mtu fursa ya kujitoa maisha yake yote kuwahudumia wale wenye uhitaji), utoaji, rehema, na huduma (neno ambalo pia linatafsiriwa kama kutumikia, au kusaidia). (c) Karama hizi zikitenda kazi watu moja kwa moja wanauona upendo wa Mungu kwa vitendo katika kutimizwa kwa mahitaji yao. Kupitia karama hizi wanaelewa jinsi Mungu anavyowajali. (3) Karama za Nguvu (a) H izi ni karama ambazo zinaudhihirisha Uwepo wa Mungu usio wa kawaida . (b) K arama hizi zinajumisha imani, uponyaji, miujiza, kunena kwa lugha na tafsiri za lugha. (c) Karama hizi zinapotenda kazi watu wanaona Shetani akiangushwa na kushindwa, ushindi dhidi ya uharibifu wa dhambi, na makusudi ya Mungu yakikamilika dhidi ya uovu mkuu. (d) Karama hizi zinaonyesha wazi kwamba Mungu ni halisi na anatenda kazi katika ulimwengu huu wa leo. (4) Karama za Uongozi (a) H izi ni karama ambazo zinafanya makusudi ya Mungu kwa Kanisa yajulikane na kuyaleta katika utekelezaji wake. (b) U tawala na Uongozi. Karama au huduma kama ofisi: mitume, manabii, wainjilisti, wachungaji, waalimu, wazee, mashemasi (1 Kor. 12:28; Efe. 4; 1 Tim. 3:1-12). (c) Karama na ofisi za uongozi zikitenda kazi, Kanisa linakamilishwa na kuwa tayari kwa ajili ya kutimiza utume wake wa kumtangaza Yesu kama Bwana.
4
Made with FlippingBook - Share PDF online