Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide
1 2 6 /
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
(d) Kumbuka: Ni watu wachache tu ndio wanaoitwa na Mungu na kuidhinishwa na kanisa kushikilia ofisi za uongozi wa Kikristo, lakini waamini wote katika kanisa wanatarajiwa kutumia karama zao katika huduma hai kwa wengine.
D. Kanuni za msingi za kitheolojia kuhusiana na karaza za Roho
1. Kila mwamini amepewa karama za kiroho ambazo Kanisa linahitaji ili kutimiza utume wa Kristo.
a. Mafundisho ya moja kwa moja ya Maandiko (1) 1 Wakorintho 12:7 (2) 1 Petro 4:10
b. Sitiari ya mwili wa mwanadamu (1) 1 Wakorintho 12:14-30
4
(2) Kila kiungo cha mwili ni tofauti na kina kazi yake ya kipekee, lakini kila kiungo ni muhimu ili mwili wote ufanye kazi ipasavyo. Vivyo hivyo kila mtu katika mwili wa Kristo ana karama tofauti za rohoni na ana kazi yake ya kipekee ya kufanya katika kanisa, lakini kila mtu anahitajika na karama zake ili kanisa lifanye kazi ipasavyo. c. Kugundua karama zako za rohoni: maswali manne muhimu (1) Ni nini ulicho nacho ambacho Mungu amekibariki? Unapowahudumia watu na wakakiri kusaidika au kuhudumiwa, kwa kawaida hiyo ni ishara kwamba unatumia karama za rohoni. Karama za rohoni huzaa matunda. Matokeo kwa kawaida ni ishara ya uwepo wa karama.
Made with FlippingBook - Share PDF online