Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide
/ 1 4 5
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
Somo hili linalenga kazi ya Roho Mtakatifu katika kuwawezesha watu wa Mungu kwa njia ya karama, kwa njia ya uongozi (kukaa ndani yao), kwa njia ya kuwapa nguvu dhidi ya dhambi na kuumbika kwa tabia ya Kristo (utakaso), na kwa njia ya kuwahakikishia waamini kwamba wamejumuishwa katika ushindi wa mwisho wa Mungu dhidi ya uovu (kutiwa muhuri). ³ Karama za rohoni zinatolewa ili kuliwezesha Kanisa kwa ajili ya utume. ³ “Kitu chochote, tukio lolote, au mtu yeyote anayetumika kama chombo cha Roho, au anayemdhihirisha Roho, au anayeakisi utendaji wa Roho, huyo ni karama ya rohoni” ( Baker Encyclopedia of the Bible ) . ³ Vifungu vya msingi vya Maandiko kwa ajili ya kujifunza kuhusu karama za rohoni ni Warumi 12, 1 Wakorintho 12, Waefeso 4, na 1 Petro 4. ³ Kila mwamini amepewa karama za rohoni ambazo Kanisa linazihitaji kwa ajili ya kutimiza utume wa Kristo. ³ Roho Mtakatifu peke yake ndiye anaye amua ni karama zipi kila mtu atapewa – ni karama za bure za “neema” na kwa hiyo wale wanaozipokea hawapati hadhi maalum au kuwa na ukomavu maalum wa kiroho. ³ Wakristo hawakubaliani kuhusiana na ufafanuzi wa baadhi ya karama, uhusiano kati ya karama za rohoni na vipaji vya asili, na endapo karama zote zilizoelezewa katika Agano Jipya zinapatikana leo. ³ Kukaa kwa Roho Mtakatifu ndani ya waamini kulifananishwa na Hema la Agano la Kale. ³ Roho anakaa ndani ya Kanisa lake (kwa jumla) na pia anakaa ndani ya kila mwamini (kibinafsi). ³ Roho anayekaa ndani yetu ni p araclete , yaani aliyeitwa kuwa upande wetu kama mtetezi ili kutuongoza, kutufundisha, kututia moyo, na kutuombea. ³ Utakaso ni fundisho linaloelezea kutengwa kwa ajili ya makusudi ya Mungu. Dhumuni la utakaso ni kumfanania Kristo kikamilifu. ³ Tumetengwa kwa ajili ya Mungu kupitia kuhesabiwa haki, utakaso, na kutukuzwa. Hivyo, “utakaso” ni tendo la wakati uliopita, uliopo na ujao. ³ Roho Mtakatifu daima yuko vitani dhidi ya uovu. ³ Matokeo ya kazi ya kutakasa ya Roho Mtakatifu katika maisha ya mwamini ni kuishi maisha matakatifu: kuenenda sawasawa mafundisho, maisha na mitazmo ya Kristo.
MUUNGANIKO
Muhtasari wa Dhana Kuu
4
Made with FlippingBook - Share PDF online