Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide

1 4 6 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

³ Kazi ya Roho ya kutia muhuri inatukumbusha kwamba wokovu wetu bado unakuja (wakati ujao), kwa kuwa haujatimizwa kikamilifu hadi Kristo atakaporudi na kutawala juu ya mbingu mpya na nchi mpya. ³ Ushahidi wa Roho unaelezea uhakikisho unaotolewa na Roho kwamba tumetiwa muhuri na kwamba sisi ni mali ya Kristo. Sasa ni wakati wa wewe kujadiliana na wanafunzi wenzako maswali uliyo nayo kuhusu karama za rohoni, kukaa kwa Roho ndani yetu, na kazi ya Roho katika kuwatia muhuri na kuwatakasa wale walio wa Kristo. Je, una maswali gani hasa kwa kuzingatia yale ambayo umejifunza hivi punde? Labda baadhi ya maswali hapa chini yanaweza kukusaidia kuunda maswali yako mwenyewe, mahususi na muhimu zaidi. * Je kuna uwezekano wa kutokea huduma ya kweli ambayo haihusishi matumizi ya karama za rohoni? Ikiwa ndiyo, kwanini? Ikiwa hapana, kwa nini? * Nini jukumu la Mchungaji/Wachungaji katika kuwasaidia watu kutambua na kutumia karama zao za rohoni? * Je, kumewahi kutokea hali ya kutoelewana katika kusanyiko lenu kuhusu karama za rohoni? Jambo hilo lilitatuliwaje? * Tunawezaje kuepuka kuonyesha kwamba karama fulani za rohoni (kwa mfano, kutenda miujiza au kufundisha) humaanisha moja kwa moja kwamba mtu aliye nazo amekomaa kiroho? * Je, theolojia ya karama za rohoni inatoa tumaini gani kwa mtu ambaye hajasoma au ni maskini? * Je, mtu anapaswa kutafuta karama fulani mahususi za rohoni? Ikiwa ndivyo, kwa msingi gani? Ikiwa sivyo, kwa nini? * Je, kitendo cha Roho kukaa ndani yetu kina mantiki na matokeo gani kwa waamini binafsi? Ni kwa njia gani makusanyiko yetu yanapaswa kutambua, kusherehekea, na kuitikia uwepo wa Roho Mtakatifu kati yetu? * Ni ipi njia nzuri ya kushughulika na mwamini fulani katika kundi ambaye amekuwa akijihusisha mara kwa mara na aina fulani ya dhambi? Je aina ya dhambi inaweza kuamua namna tunavyopswa kushughulika nayo? Je mtazamo na tabia ya mtu vinaweza kuleta utofauti wowote katika namna ya kushughulika naye? Ikiwa ndiyo, kwa nini? Ikiwa hapana, kwa nini?

Kutendea kazi somo na Matokeo yake kwa Mwanafunzi

4

Made with FlippingBook - Share PDF online