Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide
/ 1 7 5
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
K I A M B A T I S H O C H A 1 4 Mt. Basili, Kanuni ya Imani ya Nikea, na Fundisho la Roho Mtakatifu Mch. Terry G. Cornett
Kanuni ya Imani ya kwanza ya Nikea ilitokana na Kusanyiko la kwanza la viongozi wa Kikristo duniani kote huko Nikea, Bithinia (ambayo sasa ni Isnik, Uturuki) mnamo mwaka wa 325. Kusanyiko hilo liliitishwa kushughulikia uzushi uitwao Arianism ambao ulikana uungu wa Yesu na kufundisha kwamba ni kiumbe mkuu aliyeumbwa. Baraza la Nikea, lilishutumu na kulaani imani ya Kiariani, na likapambanua lugha ambayo maaskofu wangeweza kuitumia kufundisha makanisa yao kwa habari ya Yesu alikuwa nani hasa. Zaidi ya miaka 50 baadaye, hata hivyo, Kanisa lilikabiliana na changamoto nyingine. Aina iliyorekebishwa ya uzushi wa Kiariani ilianza kurejea kwa kasi; Macedonius, mwanatheolojia wa Kiariani, alikuwa amechaguliwa kuwa Askofu wa Kostantinopoli mwaka 341. Kadhalika kulikuwa na tatizo lingine jipya lililokuwa limejitokeza: Maaskofu wengine wa Kikristo walikuwa wameanza kufundisha kwamba Roho Mtakatifu si Mungu. Hatimaye Macedonius akawa kiongozi wa madhehebu ya Pneumatomachi , ambayo msingi wao wa imani uliowatambulisha ulikuwa kwamba Roho Mtakatifu si Mungu bali ni kiumbe aliyeumbwa sawa na malaika. Walifundisha kwamba Roho Mtakatifu yuko chini ya Baba na Mwana na anafanya kazi kama mtumishi wao. Basil 1 ni mmoja wa wanatheolojia wakuu wa kale waliozungumzia na kutetea fundisho la Biblia la Roho Mtakatifu dhidi ya uzushi huu. Basil alikuwa askofu wa Kaisaria aliyeishi katika karne ya 4BK. Aliandika De Spiritu Sancto (“Kuhusu Roho Mtakatifu”) mwaka wa 374, miaka michache tu kabla ya kifo chake mwaka wa 379. Kitabu hiki kilitetea imani kwamba Roho Mtakatifu ni Mungu. Basil alifanya kazi bila kuchoka kuhakikisha Baraza jipya la Kanisa linaitishwa ili kuthibitisha fundisho hili na kuhakikisha linafundishwa makanisani. Mnamo mwaka 381, muda mchache baada za kifo cha Basili, mtaguso wa maaskofu 150 wa Kanisa la Mashariki walikusanyika katika Konstantinopoli (ambayo kwa sasa ni Instanbul, Uturuki). Mtaguso huo ulithibitisha upya ukweli kwamba Yesu ni Mungu kabisa na kisha wakaligeukia swali la Roho Mtakatifu ambalo Kanuni ya Imani ya Nikea ulikuwa haijaligusia. (Kanuni ya Imani ya kwanza ilikuwa inasomeka tu kwamba “Tunaamini katika Roho Mtakatifu”). Kwa kuzingatia Maandiko ya Basil, mtaguso huo uligeuza kauli hii rahisi kuwa aya ambayo ilielezea kwa ukamilifu zaidi nafsi na kazi za Roho Mtakatifu.
1 Basil alizaliwa mwaka wa 329, katika eneo la Ponto (Uturuki ya sasa), katika familia tajiri na ya ajabu sana. Babu yake, baba yake, mama yake, dada yake na wadogo zake wawili hatimaye waliitwa watakatifu na Kanisa. Alipata elimu bora katika shule za Kaisaria, Kostantinopoli, na Athene. Kufuatia elimu yake, Basil alikua mtawa wa kwanza huko Ponto, kisha mwangalizi (nafasi ya kichungaji) huko Kaisaria (ambapo hatimaye akawa askofu) na akatokea kuwa mwanatheologia hodari pia. Katika majukumu haya, alikuza sifa ya uadilifu binafsi na huruma kubwa. Hata wakati akiwa askofu alimiliki nguo moja tu ya ndani na vazi moja la nje na hakula nyama mezani pake. Aliishi maisha rahisi, aliutesa mwili wake, na alihusika yeye mwenyewe katika ugawaji wa mahitaji kwa maskini. Kwa sababu ya uadilifu wake binafsi wapinzani wake wengi wa kitheolojia kwa miaka mingi walikuwa na wakati mgumu sana kupata chochote kibaya cha kumshtaki
Made with FlippingBook - Share PDF online