Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide
1 9 0 /
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
Maeneo Ambayo Wakristo Wanatofautiana Kuhusiana na Karama za Rohoni (muendelezo)
B. Mtazamo wa 2 – Karama za rohoni ni uwezo mpya usio wa kawaida unaotolewa kwa Wakristo ambao unapatikana kwetu tu kupitia nguvu za Mungu na unaweza kutimiza mambo yaliyo mbali sana na uwezo wa mwanadamu. Mtazamo huu unakusudia kulinda ukweli kwamba:
1. Wokovu unaweza kubadilisha na kurejesha.
2. Mungu anaweza kutoa chochote kinachohitajika katika mazingira fulani bila kujali rasilimali tunazoonekana kuwa nazo. Tunamtegemea Roho wa Mungu, si rasilimali zetu wenyewe.
3. Nguvu zisizo za kawaida zinazozidi chochote kinachowezekana katika uumbaji wa asili zinapatikana katika mwili wa Kristo.
4. Sisi sote tumeagizwa kutafuta karama fulani za rohoni ambazo zina manufaa kwa mwili (1 Kor. 12:31 & 14:12). Karama daima hutajwa kwa kurejelea jinsi zinavyotumika kuujenga mwili wa Kristo. Hakuna mahali katika Maandiko ambapo karama za rohoni zinatajwa nje na matumizi yake katika utendaji kazi ndani ya Kanisa na kupitia Kanisa. a. 1 Wakorintho 1:26-29 – Maana, ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa; 27 bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu; 28 tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko; 29 mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu.
Made with FlippingBook - Share PDF online