Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide

/ 1 9 1

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

Maeneo Ambayo Wakristo Wanatofautiana Kuhusiana na Karama za Rohoni (muendelezo)

b. Wasio Wakristo wana vipaji kupitia neema ya kawaida ( common grace )… lakini hivi ni vipaji, sio karama. Hakuna asiyeamini aliye na karama ya rohoni. Waamini pekee ndio wamejaliwa karama za rohoni…. Vipaji vinategemea nguvu za asili, karama hutegemea uwezesho wa kiroho. (Leslie B. Flynn, 19 Gifts of the Spirit).

C. Mtazamo wa 3 – Mtazamo wa kati ambao unaonyesha kwamba karama za rohoni zinaweza kuwa ama kuhuishwa na kutiwa nguvu kwa vipaji vya asili vilivyotolewa na Mungu au kuumbwa kwa vipaji vipya kabisa.

1. Kumbuka kwamba kimantiki, angalau, si lazima kwa maoni haya mawili kukinzana. Angalau inawezekana kwamba aina zote mbili za karama za kiroho zipo, zingine ambazo zipo ila zimefichwa ndani ya mtu na zingine ni mpya.

2. Pengine njia yenye manufaa zaidi ya kufikiria kuhusu hili itakuwa kukumbuka kwamba karama ni “udhihirisho” wa Roho kwa manufaa ya wote.

3. Mkazo zaidi hapa ni kudhihirishwa kwa Roho na si namna ambayo udhihirisho huo unatokea. Hili linapotokea daima huwa ni “kipawa cha neema”. Mara zote hutokea kwa sababu tu ya uamuzi wa Roho na kwa sababu ya nguvu zake. Kwa hivyo, ikiwa Roho atachagua kuwezesha uwezo wa asili au kuunda mpya kabisa, kila moja ni “ charisma ” – kipawa cha neema. Uwezo wa kufundisha unaotumiwa na mtu asiye mwamini alipewa na Mungu na ni kipawa cha neema (iliyotolewa na Roho katika uumbaji), lakini sio “udhihirisho wa Roho” hadi mtu huyo ajinyenyekeze kwa Roho Mtakatifu na kutumia karama hiyo chini ya maelekezo na kwa makusudi yake.

Made with FlippingBook - Share PDF online