Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide
1 9 2 /
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
Maeneo Ambayo Wakristo Wanatofautiana Kuhusiana na Karama za Rohoni (muendelezo)
II. Je Karama Zote Zilizoorodheshwa katika Agano Jipya Zinapatikana leo?
A. Baadhi ya mapokeo (imani za madhehebu) hujibu “Hapana.”
1. Baadhi ya mapokeo yanabishana kuhusu kukoma kwa karama fulani: kwa kawaida utume, unabii, lugha na tafsiri (wakati fulani miujiza).
2. Kuna angalau sababu mbili za kitheolojia kwa nini inaaminika hivyo.
a. Kwanza, kuna wasiwasi wa kulinda ufunuo wa Mungu katika Maandiko. Ikiwa mitume, manabii, na lugha vitaendelea kufanya kazi kama njia ya ufunuo unaoendelea, uadilifu wa Maandiko unaweza kuwekwa hatarini. Tena na tena katika historia ya Kanisa, watu wametokea ambao walidai wamepata ufunuo mpya wa kinabii ambao ulipingana na Maandiko au hata kwenda nje sana ya mafundisho yake. Ushuhuda wa kimaandiko juu ya Yesu kama Neno la mwisho la Mungu haupaswi kupotoshwa, na mapokeo haya ya kitheolojia hayaoni njia ya kupatanisha uwezekano wa mafunuo mapya na ukweli huo. b. Pili, jukumu la mitume kama “msingi” wa Kanisa linaonekana kuashiria nafasi ya kipekee katika historia ya Kanisa. Vitabu vya Injili na kitabu cha Matendo ya Mitume vinaonekana kama msingi wa historia ambapo Mungu anafanya kazi ya kipekee na bila kurudia kubadilisha ufunuo wake kutoka Agano la Kale hadi Agano Jipya. Hili linatimizwa kwa kutoa mafunuo mapya (ambayo yanaunda Maandiko ya Agano Jipya) na ishara na maajabu ambayo yanathibitisha na kuwekea msingi ushuhuda huu kuwa wa kweli. Kanisa sasa linapaswa kuishi kwa ushuhuda
Made with FlippingBook - Share PDF online