Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide
/ 1 9 5
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
K I A M B A T I S H O C H A 2 0 Kazi ya Roho Mtakatifu katika Uongozi wa Kiroho Terry G. Cornett
Kwa njia ya Roho Mtakatifu, Mungu amejiweka karibu na waamini ili waweze kuwa katika uhusiano wa kudumu, wa urafiki pamoja naye, wakipokea mwongozo na maelekezo endelevu kuhusu kile anachotaka kutoka kwao.
I. Maandiko ya Msingi
A. Warumi 8:14 – Kwa maana wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu hao ndio wana wa Mungu.
B. Isaya 63:10-14 –Lakini wakaasi, wakamhuzunisha Roho yakeMtakatifu; kwa hiyo akawageukia, akawa adui, akapigana nao. 11 Ndipo alipozikumbuka siku za kale, za Musa, na watu wake, akisema, Yuko wapi yeye aliyewapandisha toka baharini pamoja na wachungaji wa kundi lake? Yuko wapi yeye aliyetia kati yao Roho yake Mtakatifu? 12 Aliyewaongoza kwa mkono wake mtukufu, kwa mkono wa kulia wa Musa? Aliyeyatenga maji mbele yao, ili ajifanyie jina la milele? 13 Aliyewaongoza vilindini, kama farasi jangwani, wasijikwae? 14 Kama ng’ombe washukao bondeni, Roho ya BWANA ikawastarehesha; ndivyo ulivyowaongoza watu wako, ili ujifanyie jina lenye utukufu. C. Yohana 10:1-5 – Yesu aliwaambia, Amin, amin, nawaambieni, Yeye asiyeingia mlangoni katika zizi la kondoo, lakini akwea penginepo, huyo ni mwizi naye ni mnyang’anyi. 2 Aingiaye mlangoni ni mchungaji wa kondoo. 3 Bawabu humfungulia huyo, na kondoo humsikia sauti yake; naye huwaita kondoo wake kwa majina yao, na kuwapeleka nje. 4 Naye awatoapo nje kondoo wake wote, huwatangulia; na wale kondoo humfuata, kwa maana waijua sauti yake. 5 Mgeni hawatamfuata kabisa, bali watamkimbia; kwa maana hawazijui sauti za wageni.
D. Yohana 14:25-26 – Hayo ndiyo niliyowaambia wakati nilipokuwa nikikaa kwenu. 26 Lakini huyoMsaidizi, huyoRohoMtakatifu, ambayeBaba atamtuma kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.
Made with FlippingBook - Share PDF online