Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide

1 9 6 /

M U N G U R O H O M T A K A T I F U

Kazi ya Roho Mtakatifu katika Uongozi wa Kiroho (muendelezo)

E. Yohana 16:13 - Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.

F. Mdo 16:7-8 -Walipofika kukabili Misia wakajaribu kuenda Bithinia, lakini Roho wa Yesu hakuwapa ruhusa, 8 wakapita Misia wakateremka kwenda Troa (linganisha na Matendo 20:22-23).

II. Kwanini Uongozi wa Roho Mtakatifu ni Muhimu Sana?

Mkristo, anatambua kwamba anapokabiliwa na machaguo mbadala kati ya mema na mabaya, hakuna chaguo jingine; lazima mtu atende mema. Lakini changamoto kubwa zaidi inakuja tunapokabiliwa na machaguo mengi mbadala ambayo yote kimaadili ni mazuri. Sasa swali linakuwa, je ni lipi jema ambalo Mungu ananiita kufanya? Na hapo hilo lililo jema linakuwa adui wa lile lililo bora, kwani inawezekana kabisa kwetu kuzijaza siku zetu kwa mambo mema lakini tukipuuzia jambo moja ambalo ni lazima tulifanye na ambalo tumeitiwa… Kila chaguo, basi, linakuwa “ndiyo na hapana”.… Kama nitachagua kuchukua jukumu hili au kazi hii, maana yake ni kukataa fursa zingine. Ikiwa nitachagua kutumia siku yangu kwa njia hii, inamaanisha kwamba ninasema hapana kwa shughuli zingine ambazo huenda zingeijaza siku yangu. Na hakika hii ndiyo inafanya maamuzi kuwa magumu na yenye changamoto: hatuwezi kuwa kila mahali na hatuwezi kufanya kila kitu. Kuna mambo mengi mazuri ambayo tunaweza kufanya, na hatuwezi kuyafanya yote. Niseme tena, kama isingekuwa kwa sababu ya wema na utunzaji wa Mungu kwetu, hili lingekuwa mzigo wa kuogofya na usiowezekana. Yeye ni Mungu aliyepo na Aliye Hai katika vyote vilivyopo–ardhi, bahari, na anga–lakini pia ni Mungu ambaye yuko kibinafsi ndani ya kila mmoja wetu. Hatuko peke yetu! Hii ni habari njema sana.... Tunapofanya maamuzi, Roho yu pamoja nasi. Hakika tunazungumza juu ya Mungu kama Mchungaji, yaani, kama Kiongozi (Zab. 23). Na tunapata maongozi haya kwa ukaribu tunapokabiliana na nyakati zetu za kuchagua. Hata hivyo, kufanya maamuzi ni jukumu letu; ni kitendo chetu cha kufanya maamuzi ya namna tutakavyoitikia mbele ya machaguo, matatizo, na fursa ambazo zimewekwa mbele yetu. Mungu hatuchagulii, na hatuwezi kutarajia wengine wafanye maamuzi kwa niaba yetu, ikiwa kweli tunataka kukubali jukumu la utu-uzima katika maisha yetu. Hakika uwezo wa kupambanua vyema na kufanya

Made with FlippingBook - Share PDF online