Mungu Roho Mtakatifu, Mwongozo wa Mkufunzi, Capstone Module 14, Swahili Mentor Guide
2 3 0 /
M U N G U R O H O M T A K A T I F U
ubatizo wa Yesu ambapo Baba anazungumza na Roho anashuka wakati huo huo Yesu anapobatizwa, au kwa kutazama kusulubishwa kwake ambapo Yesu anahisi kuwa ameachwa na uwepo wa Baba. Katika matukio haya na mengine tunamuona Baba, Mwana, na Roho wakihusiana baina yao, jambo ambalo wasingeweza kufanya kama wangekuwa Nafsi moja katika majukumu tofauti). Waelekeze wanafunzi wafikirie na kujadili machache kuhusiana na vielelezo hivi na namna vinavyotusaidia au kufanyika vikwazo kwetu katika kufikiri kwa usahihi kumhusu Mungu. Kauli ya Mpito kuingia katika somo: “Somo letu la leo litatusaidia kugundua nafasi ya Roho Mtakatifu katika maisha ya Utatu. Tutajaribu kutafuta njia za kuelezea tofauti kati ya Mwana wa Mungu na Roho wa Mungu na tutajaribu kugundua njia ambazo Roho anahusiana na Baba na Mwana. Baadhi ya mawazo haya yatakuwa magumu kwa sababu tunazungumza juu ya fumbo kuu, lakini Kanisa limejifunza kutokana na uzoefu jinsi ilivyo muhimu kufikiria ipasavyo kuhusu asili ya Mungu na kusahihisha mawazo yasiyo sahihi kila yanapotokea. Haijalishi ni kwa kiwango gani mawazo hayo ya kitheolojia kuhusu Utatu yalivyo magumu, tunapaswa kukumbuka kwamba kweli za msingi zaidi za Utatu zaweza kupatikana kwa kukariri Kanuni ya Imani ya Nikea ambayo inaelezea kweli muhimu kuhusu asili ya Mungu katika aya chache tu.” Kanuni ya Utatu inaweza kuelezewa kwa maneno matatu: Umoja, Utofauti, na Usawa. Kila mmoja wa washirika watatu wa Utatu anajumuisha Mungu mmoja, na mmoja tu. Kuna umoja kamili, usiovunjika kati ya Mungu Baba, Mungu Mwana, na Mungu Roho Mtakatifu. Mungu ni mmoja. Kuna Uungu Mmoja tu (mitaguso ya Kanisa ilisema Baba, Mwana, na Roho ni wa “kiini kimoja,” wenye asili moja isiyobadilika). Fundisho la Utatu linalinda umoja wa Mungu. Lakini pia kuna utofauti. Mungu amejidhihirisha katika Maandiko kama aliye changamani na wa ajabu. Mungu Muumba wa ulimwengu asiye na mwisho haeleweki kwa urahisi (au kikamilifu) katika akili za wanadamu. Huyu Mungu, ndani yake, yuna namna mbalimbali. Baba si Mwana wala Roho, Mwana si Roho wala Baba, Roho si Baba wala Mwana. Mitaguso ya Kanisa ilielezea kweli
7 Ukurasa 20 Kipengele I-B-3
Made with FlippingBook - Share PDF online